Maziwa makubwa ya Amerika Kaskazini

(Elekezwa kutoka Great Lakes)

Maziwa makubwa ya Amerika Kaskazini ni jumla ya maziwa matano yanayopatikana mfululizo kwenye mpaka kati ya Marekani na Kanada. Ziwa Michigan pekee limo ndani ya Marekani tu.

Maziwa makubwa kati ya Marekani na Kanada.

Kwa pamoja maziwa hayo ni gimba kubwa la maji matamu duniani. Eneo lake linatosha kwa kuonekana kwa maji kujaa na kupwa.

Maziwa haya ni:

Maziwa makubwa jinsi yanavyoonekana kutoka angani.

Maji hupita kuanzia Ziwa Superior na Ziwa Michigan kwenda Ziwa Huron; halafu kupitia mto Detroit kwenda Ziwa Erie; halafu kupitia maporomoko ya Niagara kwenda Ziwa Ontario; kutoka huko yanafuata Mto Saint Lawrence unaokwisha kwenye Bahari ya Atlantiki.

Kuna visiwa zaidi ya 35,000 ndani ya maziwa hayo. Kisiwa cha Manitoulin katika ziwa Huron upande wa Kanada ni kisiwa cha ziwani kikubwa kuliko vyote duniani chenye eneo la km² 2,766 na eneo hili ni kubwa kuliko maeneo ya Unguja (km² 1,658) na Pemba (km² 980) pamoja.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Maziwa makubwa ya Amerika Kaskazini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.