Tumbusi
(Elekezwa kutoka Gypaetus)
Tumbusi | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Nusufamilia 2, jenasi 9 za tumbusi:
|
Tumbusi au tai mzoga ni ndege wakubwa wa nusufamilia Aegypiinae na Gypaetinae katika familia Accipitridae ambao hula mizoga. Wana mnasaba na tai. Huko Amerika kuna ndege wafananao na tumbusi, lakini wale hawana mnasaba sana na huwekwa katika familia Cathartidae. Tumbusi huvumbua mizoga kwa macho, lakini wale wa Marekani wananusa vizuri pia.
Spishi nyingi za tumbusi zina kichwa bila manyoya. Sifa bainifu hii imekua kuzuia manyoya ya kichwa yasichafuliwe kwa damu wakati tumbusi akiingiza kichwa chake ndani ya mzoga. Kichwa chenye upara kinaweza kusafishwa kwa urahisi ndani ya mto au ziwa.
Spishi za Afrika
hariri- Aegypius monachus, Tumbusi Mweusi (Cinereous, Eurasian Black au Monk Vulture)
- Gypaetus barbatus, Tumbusi Mlakondoo (Lammergeier or Bearded Vulture)
- Gypaetus b. barbatus, Tumbusi Mlakondoo wa Eurasia (Eurasian Lammergeier or Bearded Vulture)
- Gypaetus b. meridionalis, Tumbusi Mlakondoo wa Afrika (African Lammergeier or Bearded Vulture)
- Gypohierax angolensis, Tumbusi-miwese (Palm-nut Vulture)
- Gyps africanus, Tumbusi Mgongo-mweupe (White-backed Vulture)
- Gyps coprotheres, Tumbusi Kusi (Cape Vulture)
- Gyps fulvus, Tumbusi wa Ulaya (Eurasian Griffon Vulture)
- Gyps rueppellii, Tumbusi-mbuga (Rüppell's Vulture)
- Necrosyrtes monachus, Tumbusi Kapuchini (Hooded Vulture)
- Neophron percnopterus, Tumbusi Uso-njano (Egyptian Vulture)
- Torgos tracheliotus, Tumbusi Ngusha (Nubian or Lappet-faced Vulture)
- Trigonoceps occipitalis, Tumbusi Kichwa-cheupe (White-headed Vulture)
Spishi za mabara mengine
hariri- Gyps bengalensis (White-rumped Vulture)
- Gyps indicus (Indian Vulture)
- Gyps himalayensis (Himalayan Vulture)
- Gyps tenuirostris (Slender-billed Vulture)
- Sarcogyps calvus (Red-headed Vulture)
Picha
hariri-
Tumbusi mweusi
-
Tumbusi mlakondoo
-
Tumbusi-miwese
-
Tumbusi mgongo-mweupe
-
Tumbusi kusi
-
Tumbusi wa Ulaya
-
Tumbusi-mbuga
-
Tumbusi kapuchini
-
Tumbusi ngusha
-
Tumbusi kichwa-cheupe
-
Indian white-rumped vulture
-
Indian vulture
-
Himalayan griffon vulture
-
Red-headed vulture