Hafni ni elementi na metali ya mpito yenye namba atomia 72 katika mfumo radidia. Jina latokana na "Hafnia" jina la Kilatini la mji wa Kopenhagen ilipogunduliwa mara ya kwanza.

Hafni (hafnium)
Jina la Elementi Hafni (hafnium)
Alama Hf
Namba atomia 72
Mfululizo safu Metali ya mpito
Uzani atomia 178.49
Valensi 2, 8, 18, 32, 10, 2
Densiti 13.31 g/cm³
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 2506 K (2233 °C)
Kiwango cha kuchemka 4876 K (4603 °C)
Asilimia za ganda la dunia 4.9 * 1-4 %
Hali maada mango

Kutokea hariri

Hafni hutokea ndani ya mitapo ya zirkoni tu. Uzalishaji wote duniani hauzidi tani 100 kwa mwaka. Hivyo bei yake ni juu.

Haitokeo katika mwili wa kibinadamu na hakuna habari ya kwamba ni sumu ndani yake.

Tabia hariri

Rangi ni nyeupe-kijivu ikisafishwa. Haimenyuki kirahisi haivyo inatafutwa kwa aloi ambako kiasi kidogo chake huongeza uimara.

Hafni ina pia uwezo mkubwa wa kufyonza neutroni hivyo hutumiwa kwa nondo za kuendesha tanuri nyuklia.

Ikiwaka inatoa mwanga kali hivyo kuna matumizi katika mmweko wa picha.

  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hafni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.