Halima Yakoy Adam

mtu aliyeangaziwa katika UNFPA na mwanaharakati

Halima Yakoy Adam (alizaliwa karibu na mwaka 2000 katika kisiwa kimojawapo cha ziwa Chad) ni mwanasheria mshirika kutoka Chad. Akiwa amelewa na kufungwa kwenye kifaa cha mlipuko, alilazimishwa kuingia sokoni huko Bol, Chad tarehe 22 Desemba 2015. Alipoteza miguu miwili, lakini aliishi. Baada ya kupata mazoezi ya urekebishaji, alisoma ili aweze kuwa mwanasheria mshirika. Baada ya hapo, amefanya kazi kusaidia wanawake wengine walionusurika na ukatili nchini Chad.

Maisha hariri

Halima Yakoy Adam alipokuwa na umri wa miaka kumi na tano, mume wake alikuwa ni mmoja wa kikundi cha kigaidi cha Boko Haram,[1] alimpeleka katika kisiwa karibu na Mpaka wa Nigeria. Alimwambia wanakwenda kwenye matembezi ya kuvua samaki. Ilifahamika kwamba alimpeleka hadi katika kambi ya mafunzo ya kikundi cha kigaidi cha Boko Haram, ambapo alilazimishwa kuwa mshambuliaji wa kujitoa muhanga. Baada ya kupewa dawa za kulevya, alifungiwa kifaa cha mlipuko na baada ya hayo, tarehe 22 Desemba 2015 alitumwa katika soko lenye watu wengi huko Bol, Chad upande wa Chad ya magharibi.Wasichana wengine wawili walilipua mabomu yao na kupoteza maisha yao, na Yakoy Adam alipoteza miguu yake. Hata hivyo, yeye mwenyewe aliokolewa kwa wakati.[2][3]

Baada ya kupona afya yake, alirudi nyumbani kwenye kisiwa cha Ngomirom Doumou katika Ziwa Chad. UNFPA ilikuwa na uwepo kwenye visiwa hivi, na programu za kusaidia waathirika wa ukatili wa kijinsia na waathirika wa Boko Haram. Yakoy Adam alipokea huduma na urekebishaji, na alipata mafunzo ya kuwa mwanasheria msaidizi huko Bol.[3] Katika nafasi hii, anafanya kazi kusaidia wanawake wengine walionusurika dhidi ya ukatili nchini Chad,[2] na anapigania dhidi ya itikadi kali na ukatili mkali.

Amina J. Mohammed, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alimpongeza Yakoy Adam kwa ujasiri wake: Halima amebadilika kutoka kuwa muathirika hadi mpambanaji kwa sababu anatumia uzoefu huo kuwaelimisha wasichana wengine."

Marejeo hariri

  1. "https://reliefweb.int/report/niger/ending-violence-against-women-girls-sahel-crucial-sustainable-development". 
  2. 2.0 2.1 Luchsinger, Gretchen; Jensen, Janet; Jensen, Lois; Ottolini, Cristina (2019). Icons & Activists. 50 years of people making change. New York: UNFPA. uk. 146. ISBN 978-0-89714-044-7. 
  3. 3.0 3.1 "From human bomb to paralegal, Boko Haram survivor helps heal her community". www.unfpa.org (kwa Kiingereza). 
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Halima Yakoy Adam kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.