Hanaa ya Jauza
Hanaa ya Jauza (ar., lat. & ing. Alhena pia γ Gamma Geminorum [1], kifupi Gamma Gem, γ Gem) ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Mapacha (pia: Jauza, lat. Gemini) na nyota angavu ya 43 kwenye anga ya usiku.
(Gamma Geminorum, Alhena) | |
---|---|
Kundinyota | Jauza (pia: Mapacha) (Gemini) |
Mwangaza unaonekana | 1.9 |
Kundi la spektra | A1 IV |
Paralaksi (mas) | 29.84 ± 2.23 |
Umbali (miakanuru) | 109 |
Mwangaza halisi | -0.68 |
Masi M☉ | 2.8 |
Nusukipenyo R☉ | 3.3 |
Mng’aro L☉ | 123 |
Jotoridi usoni wa nyota (K) | 9260 |
Majina mbadala | 24 Geminorum, BD+16°1223, FK5 251, GCTP1539.00, HIP 31681, HD 47105, HR 2421, SAO 95912 |
Jina
Hanaa ya Jauza inayomaanisha “alama ya pacha” ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [2]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema الهنعه al-han’a inayomaanisha „ alama "[3].
Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali jina la Kiarabu na kuorodhesha nyota hii kwa jina la "Alhena" [4] .
Gamma Geminorum ni jina la Bayer kwa sababu Gamma ni herufi ya tatu katika Alfabeti ya Kigiriki na Hanaa ya Jauza ni nyota angavu ya tatu katika Mapacha (pia: Jauza - Gemini).
Tabia
Hanaa ya Jauza iko kwa umbali wa mwakanuru takriban 101 kutoka Jua letu. Ina mwangaza unaoonekana wa mag 1.7 na mwangaza halisi ni mag -0.72. Spektra yake ni ya aina ya B6[5] au B7 [6]. "B" inamaanisha ni nyota ya safu kuu inayoyeyunganisha hidrojeni (hydrogen fusion) kuwa heliamu; inawezekana imeshafika tayari mwisho wa hatua hii na itahamia karibuni kuyeyunganisha heliamu kuwa elementi nzito zaidi.
Kama nyota nyingi zinazofanana nayo inazunguka haraka kwenye mhimili wake kwa kasi ya angalau kilomita 236 kwa saa katika kanda ya ikweta yake.[7]
Tanbihi
- ↑ Geminorum ni uhusika milikishi (en:genitive) wa "Gemini" katika lugha ya Kilatini na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa, Beta, Gamma Geminorum, nk.
- ↑ ling. Knappert 1993
- ↑ Hii ni alama kama mhuri unaochomwa katika ngozi ya wanyama wa kufugwa kama ngamia, ng’ombe katika desturi ya Waarabu
- ↑ Naming Stars, tovuti ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (Ukia), iliangaliwa Novemba 2017
- ↑ Gray, R. O.; et al. (July 2006), uk. 51 (HIP 109268)
- ↑ Malagnini, M. L.; Morossi, C. (November 1990), uk. 1018 (HD 209952)
- ↑ Kaler, Al Nair
Viungo vya Nje
- Constellation Guide:Gemini
- Gemini, kwenye tovuti ya Ian Ridpath, Star Tales, iliangaliwa Oktoba 2017
- ALHENA (Gamma Geminorum), kwenye tovuti ya Prof Jim Kaler, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017
Marejeo
- Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 331 (online kwenye archive.org)
- Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331