Mng'aro wa Jua
Mng'aro wa Jua (kwa Kiingereza: solar luminosity ) ni jumla ya mng'aro au mnururisho wa sumakuumeme unaotoka kwenye Jua na kuelekea nje yake katika anga-nje pande zote. Hii ni pamoja na wimbiredio, mikrowevu, mawimbi ya joto, eksirei, na nuru inayoonekana kwetu.
Mng'aro huo huwa na kiwango cha nishati cha Joule 1367 kinachofika kwa kila mita ya mraba katika umbali wa kizio astronomia moja (= kilomita milioni 150, sawa na umbali wa Dunia kutoka Jua).
Hali halisi ni kwamba kiwango cha nishati kutoka Jua kinachofika kwenye uso wa ardhi kinaweza kuwa chini yake; maana uso wa Dunia haukai wima kwa Jua bali unainama kwa pembe fulani inayobadilika katika mwendo wa mwaka; mabadiliko ya pembe ya mng'aro wa Jua ndiyo sababu ya kuwa na majira ya joto na baridi duniani.
Mng'aro wa Jua kama kipimo cha astronomia
Kiasi cha nishati ya Jua kinachofika kwa umbali wa kizio astronomia moja, yaani takriban kwa umbali wa Dunia kutoka Jua, kinatumiwa kama kipimo cha ulinganishi wa nyota.
Hapo mnururisho wote wa nyota unaopimwa unalinganishwa na mng'aro wa Jua. Alama yake ni .
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mng'aro wa Jua kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |