Halfan Hythani Hamza (maarufu kama Hassan Mwakinyo; alizaliwa 15 Machi 1995 mkoani Tanga) ni mtaalamu wa mchezo wa masumbwi na ngumi za kulipwa kutoka nchini Tanzania. Ni mwanamasumbwi wa uzito wa kati. Mpaka mwaka 2018 Mwakinyo alikuwa anashika namba 235 kidunia na namba 1 barani Afrika katika ndondi za uzito wake.[1]

Amekuwa akijihusisha na mchezo wa masumbwi tangu mwaka 2015 akiwa na umri wa miaka 20. Ana kimo cha futi 5 na inchi 8.

Marejeo hariri

  1. https://boxrec.com/en/proboxer/742000