Helmut Heinrich Waldemar Schmidt (Hamburg, 23 Desemba 1918 - Hamburg, 10 Novemba 2015) alikuwa mwanasiasa wa Kijerumani na pia alikuwa chancela wa Shirikisho la Jamhuri ya watu wa Ujerumani kuanzia 1974 hadi 1982.

Helmut Schmidt (1977)

Helmut Schmidt alizaliwa mjini Hamburg mnamo 1918. Alimaliza shule yake mnamo 1937. Baada ya hapo akawa anafanya kazi katika makampuni kadhaa na baadaye akaja kujiunga na jeshi. Mwishoni mwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia alikuwa Luteni wa kwanza kuchaguliwa kwa nchi ya Ujerumani tangu vita kwisha. Pia alishawahi kuwa mfungwa wa vita kunako mwaka wa 1945.

Baada ya kuachiwa huru akarudi tena masomoni na akaanza kusomea mambo ya uchumi. Alihitimu masomo yake hayo kunako mwaka wa 1949. Baada ya hapo akawa anafanya kazi ya utumishi katika mji wa Hamburg.

Alijiunga na chama cha SPD mnamo mwaka wa 1949. Mnamo 1953 akawa mwanachama wa Bundestag kwa mara ya kwanza. Kuanzia 1961 hadi 1965 alikuwa Seneta wa jimbo la serikali la Hamburg.

Kuanzia 1969 hadi 1972 alikuwa Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani ya Magharibi, na kuanzia 1972 hadi 1974 alikuwa Waziri wa Fedha.

Baada ya Willy Brandt kuachia ngazi kuwa kama Bundeskanzler, Helmut Schmidt akachaguliwa kuwa chancela mpya wa Ujerumani.

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Helmut Schmidt kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.