Hibo Wardere
Hibo Wardere ni mwanaharakati wa mapambano dhidi ya ukeketaji wa wanawake (FGM), mwandishi, na msemaji wa umma mzaliwa wa Somalia. Alihamia London, Uingereza angali kijana mwaka 1989 kama mkimbizi aliyekimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Somalia. Kwa sasa anaishi Walthamstow London, ambako alifanya kazi kama mpatanishi na mwalimu wa kawaida katika misitu ya Waltham. Ushuhuda wake na kazi ya kampeni imemfanya awe miongoni wa wahamasishaji maarufu zaidi wa nchini Uingereza dhidi ya upingaji ukeketaji (FGM) na ameonekana katika machapisho mengi, ikiwa ni pamoja na Telegraph, BBC, na Guardian.
Maisha
haririHibo Warere alipokuwa na umri wa miaka sita alikuwa mwathirika wa ukeketaji ambapo alipata maumivu makali kuanzia kicwani mpaka vidole. ".[1][2].Kwa kipindi cha miaka kumi alijaribu kumuuliza mama yake kwa kilichotokea bila kupata majibu yoyote ya kuridhisha baada ya kukanusha majibu, baadae alivyofikisha umri wa miaka 16 ndipo alipoamua kupanga mpango na mwanaume ambaye alimuahidi kumwambia kila kitu baada ya usiku ya harusi, ingawa aliogopa, akakimbilia London baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kwenye miaka ya 1980.
Maisha binafsi
haririHibo Wardere anaishi na mumewe Yusuf na watoto wao saba.
Marejeo
hariri- ↑ Lytton, Charlotte (2015-02-06). "FGM survivor: 'The pain was so bad, I prayed to God to take me then and there'". Telegraph.co.uk. Iliwekwa mnamo 2016-05-14.
- ↑ Ritchie, Meabh (2016-04-24). "'This is what it's like to pee after female genital mutilation'". BBC News. Iliwekwa mnamo 2016-05-16.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hibo Wardere kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |