Hifadhi ya Tswalu Kalahari
Hifadhi ya Tswalu Kalahari ni hifadhi ya wanyama inayomilikiwa na watu binafsi katika Rasi ya Kaskazini, Afrika Kusini. Ni hifadhi kubwa binafsi ya nchini Afrika Kusini, inayochukua eneo la zaidi ya hekta 111,000. [1]
Historia
haririPori la Akiba la Tswalu liliopo kusini mwa Kalahari lilianzishwa na Stephen Boler . Alinunua makumi ya mashamba ili kuanzisha hifadhi hiyo, alianzisha wanyamapori wa Kiafrika katika makazi yao ya asili, ikiwa ni pamoja na simba, aina adimu za swala, twiga, nyati, na pundamilia.
Hifadhi hiyo ndiyo makazi ya faru wengi zaidi duniani. [2]
Marejeo
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya Tswalu Kalahari kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |