Hifadhi ya kisiwa cha Saanane
Kisiwa cha Saanane (Saanane Island National Park) ni hifadhi ya taifa la Tanzania na ni hifadhi ndogo yenye eneo la kilomita za mraba 2.18, na iko umbali wa kilometa 2 kusini magharibi kutoka katikati ya jiji la Mwanza, katika Ghuba ya Ziwa Victoria nchini Tanzania.
Hifadhi hii ilianzishwa kama bustani ya kwanza ya wanyama nchini Tanzania mwaka 1964 ikawa hifadhi kamili mwaka 2013.
Lengo la kuanzishwa kwake ilikuwa kuhamasisha uhifadhi wa wanyama na kuelimisha jamii, pamoja na kutoa nafasi kwa wakazi wa Mwanza kupumzika.
Jina la hifadhi hii lilitokana na muanzilishi wa bustani aitwaye Saanane Chawandi. Kati ya mwaka 1964 na 1966 wanyama mbalimbali walihamishiwa katika kisiwa hiki.
Wanyama hao ni pamoja na mbogo, digidigi, tembo, pofu, pongo, swala pala, ngiri, pundamilia, kima, twiga, nungunungu, mamba n.k
Wanayama wakali kama faru na mbogo walifungiwa na wanyama wapole waliachwa huru.
Bustani hii iliachwa kuwa pori la akiba mwaka 1991.
Muonekano wa Ziwa Victoria katika kisiwa cha Saanane ni kivutio kikubwa. Vilevile muonekano wa Kisiwa cha Saanane uwapo Mwanza ni kivutio kingine kikubwa.
Hifadhi hii inafikika wakati wowote katika mwaka. Na unaweza kufika kwa kutumia boti ukitokea katika mji wa Mwanza.
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- "SAANANE ISLAND DECLARED NATIONAL PARK". TANAPA. 3 Septemba 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-09-08. Iliwekwa mnamo 5 Septemba 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Nkwame, Marc (4 Septemba 2013). "Saa-Nane Island becomes fully fledged park". Daily News (Tanzania). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-09-06. Iliwekwa mnamo 6 Septemba 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - Philemon, Lusekelo (5 Septemba 2013). "Saanane Island officially declared 16th National Park". IPP Media. Iliwekwa mnamo 6 Septemba 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)* - Nkwame, Marc (8 Septemba 2013). "Rocking and rolling on Saa Nane Island Park". Daily News (Tanzania). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-09-08. Iliwekwa mnamo 9 Septemba 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)</ref>
Viungo vya nje
hariri- TANAPA
- Utalii wa Tanzania Archived 13 Januari 2010 at the Wayback Machine.
- Safiri Tanzania
- Maliasili za Tanzania
- Safari za Tanzania
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mwanza bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya kisiwa cha Saanane kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |