Historia ya Wasangu

Historia ya Wasangu inahusu kabila hilo la watu ambao inasemekana wametokana na jamii za Wahehe, Wasafwa, Wabena, Wanyakyusa na kidogo jamii ya Wangoni. Hata hivyo wengine wanasema huo ni upotoshaji mkubwa na kuna tofauti kubwa kati ya Kisangu na lugha za hizo jamii.

Kwa vyovyote, jamii hizo, isipokuwa Wangoni, ni jirani za Wasangu, ambao kwa jumla walijulikana sana katika nyanda za juu za Kusini katika karne ya 18 na karne ya 19 na walikuwa na nguvu nyingi sana katika utawala na vita.

Hawa watu walikuwa wanaishi sehemu ya llamba iliyo karibu maili 60 Kaskazini ya Utengule kabla ya kuja Waarabu na Wajerumani, na kila mahali walipofanya maskani yao walipaita "Utengule", mahali pa amani.

Waarabu walipokuwa wanaingia katika nchi ya Usangu waliingia kufanya biashara. Hawa Waarabu walikuwa wanauza nguo, magobole, baruti na shanga. Kutoka kwa Wasangu, Waarabu walipata meno ya tembo. Hapo awali mbuga zote za Usangu zilikuwa na wanyama wa kila aina na ndovu walienea kila mahali katika mbuga hizi za Usangu, kwa hiyo ilikuwa rahisi sana kwa Wasangu kuwaua tembo na kupata meno yao ili wayauze kwa Waarabu.

Biashara nyingine kubwa ambayo ilikuwa inafanywa na Waarabu katika mbuga hizi za Usangu ilikuwa biashara ya utumwa. Wasangu walikuwa ni watu ambao walijua namna ya kupigana vita sawasawa na kwa kuwa walikuwa na chifu wao mmoja tu ilikuwa rahisi kwao kuungana pamoja na kufanya jeshi moja kali na lenye nguvu sana kuliko jamii zingine walizopakana nazo ambazo zilikuwa hazina utawala mmoja kama vile Wanyakyusa, Wasafwa na kadhalika. Lakini Wahehe na Wakimbu walikuwa na utawala mmoja sawa kama Wasangu walivyokuwa.

Kwa kuwa utawala wa Wasangu ulikuwa na nguvu na umoja mkubwa, waliweza kupigana vita kwa nguvu moja na jamii zingine zilizokuwa jirani nao. Chifu Merere, ambaye ndiye aliyekuwa mtawala wa Wasangu, alikuwa mtawala shupavu na mpenda raia wake. Kwa kuwa alikuwa anapata silaha bora toka kwa Waarabu alipowauzia meno ya tembo, aliweza kuwashinda maadui zake bila taabu kubwa na mateka waliuzwa kwa Waarabu wafanya biashara ya utumwa.

Hasa Merere aliwauza utumwani watoto wa Kisafwa na Kihehe ambao aliwateka wakati wa vita. Uwezo wake Merere katika kupigana na jirani zake ulisaidiwa sana na ushauri aliokuwa anaupata toka kwa wazee wa Kisangu na pia toka Mbaluchi ambaye alikwenda Usangu na kuwa Mshauri Mkuu wa Vita wa Chifu Merere I ambaye yaaminiwaaliingia nchi ya Usangu kati yamwaka1878 na mwaka1880. Mbaluchi (Mburushi) huyu aliitwa Jemadari ambaye kufika kwake Utengule/Usangu kulisababisha Wabaluchi wengine kuja Usangu na kuanza shughuli za kilimo cha mpunga (angalia chini ya kilimo hapa chini). Wasangu wenyewe wanasimulia kuwa Waarabu walianza kuingia nchi ya Usangu wakati wa utawala wa Chifu Njali aliyewazaa akina Merere.

siri na kupita huko. Si njia ya kutoka pwani tu iliyohatarishwa na Wasangu ball hata njia ya kuelekea nchi ya Wabemba kuelekea Zambia ilitiwa msukosuko.

Mara kwa mara Wasangu waliuteka utawala wa Kiwele uliokuwa sehemu ya kati ya Ukimbu ambao ulikuwa njiani Kusini ya Tabora. Mara baada ya Chifu Kilanga kutawala katika nchi ya Ubungu, Wasangu walimshambulia katika mwaka wa 1856 — 1857 wakimsaidia ndugu yake Kafwimbi, na ingawa Wasangu walishindwa, Kafwimbi alitorokea nchi ya Usangu tena. Kati ya mwaka 1859 wakati Bwana Burton alipoondoka Afrika ya Mashariki na mwaka 1866 Tippu Tip alipotembelea reli ya Usangu chifu Muigumba akafariki wakati akipigana na Wahehe.

Binini, ndugu ya Mihwela alikuwa amejifunza sana maarifa ya kupigana vita, na kwa kuwa alikuwa na ari kubwa ya kutaka kutawala Uhehe nzima. Wakati fulani karibu ya miaka ya 1860 alifanya vita na Wasangu na alifanikiwa kuviteka vijiji vingi sana na kuwateka wanawake na mifugo yao. Binini mwenyewe alimwua kiongozi wao Muigumba na akachukua jina lake na kujiita yeye mwenyewe Munyigumba kama ukumbusho wa ushindi wa kuwatawala Wahehe wote. Huyu Binini (Munyigumba) ndiye aliyekuwa baba wa chifu Mkwawa na ndiye chifu mkuu wa kwanza wa Wahehe wote.

Baada ya kifo cha Muigumba vita vikali sana vya urithi wa utawala vikatokea na mjukuu wake Muigumba kwa jina Merere Towelamahamba akatokea kuwa mshindi na akawaua jamaa zake wengi sana ambao alishindana nao katika kurithi utawala. Ugomvi wa urithi wa utawala uliwadhoofisha sana Wasangu katika kupigana vita na majirani zao.

Kati ya mwaka wa 1866 na mwaka wa 1872 Wasangu wakatokea jamii yenye nguvu sana chini ya chifu Merere wa kwanza kuliko hapo awali, na wakawashambulia majirani zao na kuziteka nchi zao zote hasa upande wa Mashariki Kusini na upande wa katikati wa nchi ya Wakimbu. Wakati huu Wasangu walikuwa wamefikia kilele cha nguvu zao na hakuna jamii nyingine yoyote iliyoweza kuikabili jamii ya Kisangu katika pande hizo za Tanzania.

Katika mwaka wa 1867 Bwana Livingstone aliambiwa na Waarabu katika nchi ya Ubungu kwamba Wasangu walikuwa ni wapole kwa wageni wowote, na kwamba Merere mara nyingi alifanya mashambulizi kwa machifu wa jirani ili ateke mifugo na watumwa na kuwauza kwa wafanya biashara wa Kiarabu. Katika mwezi wa Agosti Bwana Livingstone alisikia habari nyingi zaidi za kupendeza kuhusu chifu Merere na alichelea kuwa huenda akaharibiwa na Waarabu.

Walakini katika mwaka wa 1871 habari zikafika Mayema kwamba Merere kisha kosana na Waarabu akiwatuhumu kwamba walikuwa wanafanya njama ya kumshambulia ili Goambari, mmojawapo wa Wajukuu wa Muigumba aweze kutawala. Kwa ajili ya sababu hii Merere akawashambulia Waarabu na marafiki zao wote.

Akamwua Mwarabu mmoja akawanyang'anya Waarabu wengine mali yote waliyokuwa nayo.

Wakati huu Amrani Masudi akajitokeza kwenye uwanja wa vita. Amrani alikuwa Mwaarabu toka Zanzibar wakati Zanzibar ilipotawaliwa na Waarabu.

Tanzania Bara ilikuwa inatawaliwa na machifu mbalimbali wa jamii mbali mbali na Waarabu waliokuwa wakiishi Tanzania Bara walikuwa wafanya biashara tu sio watawala. Kwa jinsi hii Amrani hakupendelea utaratibu huu, kwa hiyo akaamua kuwafanyia vita machifu wote wa Tanzania Bara na kuwafanya watu wote wawe chini yake ili baadaye waweze kumletea meno ya tembo bila ya kuyalipia chochote.

Wakati Amrani Masudi alipofika Tabora akaambiwa kuwa kuna machifu wawili wenye nguvu sana ambao walihatarisha misafara yote ya biashara ya Waarabu na kuwatoza kodi kubwa kabla ya kuwaruhusu kupita katika nchi zao. Machifu wenyewe ni Nyungu-ya-Mawe wa Kiwele katika nchi ya Ukimbu na Merere wa Usangu. Lakini chifu wa hatari kabisa na mwenye nguvu zaidi kuliko mwenzake alikuwa Merere.

Baada ya kupata habari hizo, Amrani akalichukuwa jeshi lake na akaomba kuongezewa askari toka kwa machifu waliomwogopa kupigana naye ili aende na jeshi kubwa la kuweza kumshambulia Merere vilivyo. Alipoondoka Tabora, alipita Ngulu, Unyangwila, Itumba, Kipembawe na Igunda mpaka akafika Usangu. Maluteni wake walipita Ukonongo, Isamba, Wikangulu, Ubungu na Uguruke. Wengine walipitia Ugogo. Kila chifu wa sehemu za Magharibi na kati na Kusini ya Tanzania alitoa kwa Amrani askari wa kumsaidia katika vita kati yake na Wasangu. Lakini Nyungu-ya-Mawe hakutoa hata askari mmoja wa kumpa Bwana Amrani.

Wasafwa kutoka sehemu za Ukinga ni kwamba nchi ya Ukinga imeinuka sana na mwinuko huu huwagawanya watu kuwa katika pande mbili zilizo tofauti ya hali ya Kijiografia, hata baadaye watu ambao pengine asili yao ni moja kuwa katika jamii mbili zilizo tofauti kabisa, ambazo lugha zao zatofautiana.

Mambo yanapotokea hivi, basi kutoelewana kwaweza kutokea na kuchukiana pia kukatokea. Ngazi hii ikifikiwa basi kundi lisilotaka ugomvi huhamia mahali pengine ambapo kuna usalama zaidi na hali hii yawezekana kabisa iliwapata Wasafwa na kuamua kuhamia sehemu za Mbeya ambako maskani yao ya kudumu yalifanyika. Jamii ya Wasafwa yagawanyika katika jamii hizi kubwa:

(i) Wasongwe ambao huishi sehemu za mto Songwe;

(ii) Wamalila ambao wanaishi katika milima ya Umalila.

(iii) Wamporoto ambao huishi kwenye milima ya Mporoto.

(iv) Wambwila ambao huishi kati ya Wasongwe na Wasangu.

(v) Waguluhaambao huishi sehemu za lleya.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Wasangu kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

[[Jamii:Historia ya Tanzania] BOMA LA CHIFU MERERE ENEO LA UTENGULE-USANGU WILAYA YA MBARALI MKOANI MBEYA.

Na hii ni orodha ya machifu wa abila la wasangu waliowahi kutawala katika himaya ya wasangu: Mui'Gumbi Merere I –(1834 - 1860), Tovelamahamba Merere II –(1860 –1893), Mgandilwa Merere III awamu ya kwanza,(1893 1896 ), Mgandilwa Merere III (1896 – 1906) (awamu ya pili), Mxabuwoga Merere IV(1906 – 1950)

Machifu wengine waliowahi kutawala ni Myotishuma (1950 – 1953) Alfeo Mgandilwa Merere V (1953 – 1962), Ahmed Merere VII 1989 – 2002, Yusuf Merere VI,(2002 – 2003) na chifu wa sasa ni - Salehe Alfeo Merere VIII(2003-mpaka sasa).

NB: MACHIFU wengine wanaotajwa kutawala katika bonde la Usangu kulingana na machapisho ya vitabu mbalimbali ni

Mgandilwa(Pambalu) Merere,1893-1906.

Tunduhwago Merere 1906 -1910

Mtenjela Merere 1911-1937

Nkanu woga Merere 1937-1950

Alfeo Merere 1950-1988

Yusufu Merere alitawala kwa Muda tu kuanzia 1988 (na anaishi Dodoma)

Ahamed Merere 1989 -2002

Salehe Alfeo Merere 2003-

Na katika eneo la Ngelyama ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kuna eneo la kufanya mila za jadi (matambiko) ambayo yaatajwa kudumi kwa zaidi ya miaka 200.

Mbali na kivutio cha Ngome ya Chifu Merere,bonde la Usangu(Mbarali) kuna vivutio vingine kama Mti mkubwa wenye historia ya kufanyika mapatano ya usuluhishi kati ya Chifu Mkwawa na chifu Merere katika kijiji cha Luwango Kata ya Ipwani baada ya mapigano ya kivita baina yao.

kuna Mabaki ya Ngome ya Wajeruman iliyopo katika kiiji cha Ibelege Kata ya Ipwani na Mlima Ngoni wenye mapango yenye simulizi uliopo katika Kijiji cha Chamoto Kata ya Igurusi.

Pia kuna Masalia ya kiwanda cha kutengenezea zana za Kale katika Kijiji cha Mlungu Kata ya Miyombweni na maji moto katika kijiji cha Udingilwa kata ya ya Luiwa.

Na katika mji wa Mbalizi wilaya ya mbeya katika eneo la Utengule kuna masalia ya Ngome ndogo ya Chifu merere ambapo utafanikiwa kuona kabuli la Chifu wa wa sangu Tovela mahamba.

LIJUE BONDE LA USANGU

BONDE LA USANGU (Usangu Valley) lililopo wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya ni eneo lenye mvuto mkubwa kutokana na kuwa na umbo la Bakuli,bonde hilo linafanana na bonde la Ngorongoro na huonekana vizuri katika safu za milima ya chunya Mkoani Mbeya umbali wa wastani wa km 20 kutoka Mbeya Mjini(Point of view of Usangu Valley).

Bonde la Usangu lina ukubwa wa eneo la Kilometa za mraba 16,000 ambapo eneo la km 6,000 ni kwajili ya makazi ya watu na eneo la km 10,000 ni sehemu ya eneo la km 20,226 za Hifadhi ya Taifa ya Ruaha baada ya serikali kupunguza eneo la makazi ya wananchi mwaka 2007-08.

Maajabu ya bonde la USANGU ni kuwa lipo uwanda wa chini wa tambarare wenye nyasi na vichaka(Savana) na sehemu kubwa ya bonde hilo imepitiwa na Bonde la UFA.

Ukiwa katika bonde hilo la Usangu ndiyo eneo pekee unaloweza kuona chanzo cha mto mkubwa wa RUAHA MKUU nchini Tanzania, ambao humwaga maji katika mto Rufiji na kisha humwaga maji katika Bahari ya Hindi.

Kuna vyanzo vya mito mikuu mitatu ya Ruaha mkuu,Mkoji na mto Mbarali(barali) ambayo ndiyo chanzo kikubwa cha shughuli za kilimo cha umwagiliaji katika eneo la Bonde hilo la Usangu.

Wastani wa Mvua katika bonde la Usangu ni kama ifuatavyo 2005/2006 milimita 300.00,2006/2007 milimita 800.00, na 2007/2008,milimita 450.00,lakini wastani wa mvua katika bonde hilo ni kati ya milimita 500-900 kwa Mwaka.

Bonde la Usangu lipo katika usawa wa mita 1,000 – 1,800 juu ya usawa wa Bahari na wastani wa joto ni kati ya nyuzi 25c na 30c kwa mwaka . na mvua ni kati ya mwezi desemba na April na bonde hilo lina uoto wa asili wa miti ya mipogoro na miti mingine yenye asili ya miiba na vichaka

Wenyeji wa Bonde hilo la Usangu ni kabila la WASANGU ambao hujishughulisha na ufugaji na kilimo cha mpunga na baadhi ya mazao mengine,lakini ni moja ya maeneo nchini Tanzania ambayo huzalishaa zao la Mpunga na sehemu kubwa ya ardhi yake haitumii mbolea kutokana na mito inayoanzia safu za milima ya kipengere,uporoto na chunya kutililisha mboji katika bonde hilo.

Ukiwa ndani ya Bonde la Uangu unaweza kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha baada ya upanuzi wa eneo la pori la Akiba la Usangu (Usangu Game Reserve) lililokuwa na kilometa za Mraba 4,148 na baadhi ya maeneo mengine ya vijijiji vya Upagama,Ukwaheri,Kiwale Sololwambo,Msangaji,Idunda katika kata ya Msangaji na Kijiji cha Ikoga ambayo pia yaliondolewa.

Pia ndani ya Bonde hilo kuna eneo Oevu la Ihefu(Ihefu Swamp) lenye mvuto mkubwa ambalo ni eneo chepechepe lenye ukubwa wa Kilometa za Mraba 80 lililopo katika hifadhi ya Ruaha na ambalo hufyonza maji kutoka mto ruaha Mkuu kabla ya kuyaruhusu kuendelea katika bwawa ya Mtela

MAAJABU YA ENEO OEVU LA IHEFU NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA RUAHA.

IHEFU ni neno linalotokana na asili ya neno la kabila la WASANGU ( LIHEFU ) lenye maana ya majani yanayotanda juu ya maji kwa kujisuka.

Majani hayo yaliyojisuka kwa ustadi wa aina yake yanauwezo wa kumwezesha mtu yeyote kutembea juu ya majani hayo huku chini kukiwa na kina kirefu cha maji yanayotembea (ingawa ni hatari kidogo).

Eneo la ihefu lililo ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha linakadiliwa kuwa na ukubwa wa kilometa za mraba 80 na ni eneo ambalo nyakati za masika hujaa maji kupitia mto Ruaha mkuu kabla ya maji hayo kwenda katika mabwawa ya mtera.

Unavyofika katika eneo la Ihefu ndani ya hifadhi ya Ruaha utastaajabu kuona mbuga kubwa sana inayovutia kwa muonekano ambayo si rahisi kuona mwisho wake kwa macho ya kawaida na na ndani kukiwa na miti michache sana ambayo huwa kinvuli kwa baadhi ya wanyama.

Ndani ya eneo hilo Oevu la Ihefu kuna wanyama wa aina mbalimbali wakiwemo pofu,Swala,ngiri, nguruwe,digidigi na viboko,lakini sehemu kubwa ya eneo hilo la Ihefu ndani ya hifadhi hiyo lina tawaliwa na makundi ya ndege aina ya Mbuni wenye maumbo makubwa kwa muonekano na wanaolandalanda kwa madaha muda wote katika eneo hilo.

Wastani wa joto katika eneo la Ihefu ni nyuzi joto 34(34C), lakini ni vigumu sana kujisikia joto au jua kali ndani ya eneo la Ihefu kutokana na hali ya hewa yenye upepo mwanana unaokufanya usichoshwe mazingira yake ambayo sehemu kubwa ni mbuga kubwa yenye miti michache sana na nyasi fupi.

Nyakati za Kiangazi ndani ya bonde hilo sehemu kubwa ya maji hukauka kutokana na hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo kwa kiasi kikubwa yamesababishwa na shughuli za ufugaji wa mifugo ikiwemo ng’ombe kabla ya eneo hilo halijawa eneo la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha .

Kabla ya serikali kuchukua uamuzi wa kuiondoa mifugo katika eneo hilo la Ihefu kati ya mwaka 2006 -2008 kutokana na uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji katika Mto Ruaha mkuu na eneo hilo Oevu la Ihefu.

Ikumbukwe kuwa eneo hilo Oevu la Ihefu(Ihefu Swamp) kabla ya kuwa sehemu ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha mwaka 2008,awali sehemu ya eneo hilo lilikuwa likifahamika kama eneo Oevu la akiba la Utengule(Utengule Swamps Game Controlled Area (USGCA) chini ya serikali ya kikoloni ya Uingereza tangu mwaka 1953 hadi Uhuru.

Na kati ya mwaka 1985 hadi 1995 serikali ya Tanzania ilianzisha jitihada zaidi za uhifadhi wa eneo hilo na mwaka 1998 serikali ilitangaza rasmi eneo hilo kuwa pori la akiba la Usangu (Usangu Game Reserve).

Na mwaka 2008,Rais wa serikali ya awamu ya Nne ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete alitembelea eneo hilo na kutoa karipio kali la kuwataka wafugaji waliobaki waondoke haraka na kwenda mikoa mengine kupisha eneo hilo la Ihefu ambalo ni sehemu ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambayo ni ya pili kwa ukubwa Barani Afrika.

JE unapenda ngoma za Kisangu? Kabila la wasangu wana ngoma zenye mvuto wa aina yake ikiwemo Ngoma ya MALENJELA,NGADULE na MYONGA

Imeandaliwa na Charles Ngwambi March 2022