Honey Smacks ni chakula cha aina ya ngano iliyofanywa kuwa tamu kinachotayarishwa na Kellog's.

Jina la Bidhaa: Honey Smacks
Kampuni inayotayarisha: Kellog's
Ilianzishwa: mwaka wa 1953
Masoko:
*. Marekani, Marekani
*.Meksiko
*.Uingereza

Kiwango cha Sukari

hariri

Katika mwaka wa 2008, ulinganisho wa thamani ya lishe za bidhaa 27 za nafaka, Ripoti za Wateja za Magazeti ya Marekani zilionyesha kuwa Honey Smacksna Golden Crisp ndizo zilikuwa na sukari nyingi katika bidhaa zao - zaidi ya asilimia 50 ya uzito wa bidhaa. Ripoti ilisema "Kuna kiwango cha sukari katika kula Honey Smacks sawa na kula ndazi la donut lililopakwa sukari la duka la Dunkin' Donuts." (Bidhaa zote mbili ni za ngano yenye imefanywa tamu) Ripoti za Wateja zilipendekeza kuwa wazazi wachagulie watoto wao bidhaa za nafaka zenye thamani kubwa ya lishe .

Historia ya masoko

hariri

Ilianzishwa katika mwaka wa 1953, bidhaa hii imebadilishwa jina mara kadhaa. Ilianza ikiitwa Sugar Smacks. Katika miaka ya 1980, iliiitwa Honey Smacks. Katika mwanzoni wa miaka ya 1990, labda kwa sababu katuni ya kuwakilisha bidhaa ,Dig'em Frog, ilionyeshwa mara kwa mara ikiita bidhaa Smacks, neno la Honey likatolewa kutoka jina la bidhaa na ikaitwa Smacks. Katika mwaka wa 2004, bidhaa hii ilipewa jina lake la awali na likaitwa Honey Smacks na hili ndilo jina lake hadi sasa. Katika nchi ya Meksiko inajulikana kama SMAK.

Kaulimbiu kadhaa zimetumika katika kutangaza Honey Smacks kwa mfano: They're Honey Smackin' good!" kutoka mwaka wa 1984-1987, "I Dig'em" katika mwaka wa 1991-1994, na "Satis-Smack-tion!" (1995-1997).

Watumbuizaji wanaojulikana kama clown wametumika ,pia, katika kutangaza bidhaa hii kutoka mwaka wa 1953 mpaka 1956 kwa mfano Cliffy the Clown alitumika katika matangazo. Katika mwaka wa 1957 , mnyama wa kuogolea majini anajulikana kama seal aliyevaa sare za baharia ndiye aliyekuwa mwakilishi wa bidhaa hii. Katuni farasi ya Hanna-Barbera iliyoitwa Quick Draw McGraw ikawa mwakilishi katika mwaka wa 1961 na ikafuatiwa na The Smackin' Bandit katika mwaka wa 1965. Alibadilishwa katika mwaka wa 1966 na Smackin' Brothers waliokuwa kaka wawili waliovaa kaptula za dondi na kinga za dondi. Mwanzoni mwa miaka ya 1970, Chifu Mhindi alikuwa mwakilishi kwa muda mfupi na akabadilishwa na Dig 'Em Frog katika mwaka wa 1972. Dig 'Em aliendelea kuwa katuni mwakilishi wa bidhaa hiyo hata baada ya kubadilishwa jina kuwa Honey Smacks. Dig 'Em alibadilishwa na mnyama anayehusiana zaidi na asali, Wally Dubu, katika mwaka wa 1986, lakini Dig 'Em akarudishwa kwa sababu ya mahitaji ya umma katika mwaka wa 1987. Katika miaka ya 1990, matangazo ya kampeni kwa ajili ya bidhaa hi ilihusisha Dig 'Em akijaribu kula Smacks ilhali akimhepa adui wake, Kitty. Katika mwaka wa 1997, matangazo hayo yakaacha kutangazwa.

Katika Uingereza, bidhaa hii iliwakilishwa na kutangazwa na katuni Barney Bee na ikashindana na bidhaa ya Sugar Puffs kutoka kampuni ya Quaker's. Hata hivyo, kutokana na umaarufu wa Sugar Puffs,hivi sasa inajulikana kama Puffa Wheats, Honey Smacks hupatikana katika Poundland na maduka mengine ya Pound katika Uingereza.

Katika Australia, bidhaa hii imejulikana kama Honey Smacks tangu miaka ya 1970. Huko Unorwe, bidhaa hii inajulikana kama "Honni Korn Smacks".

Marejeo

hariri
  1. ^ Better cereal choices for kids? Some child-focused products are 50 percent sugar consumerreports.org

Viungo vya nje

hariri