Kaka ni jina ambalo linatumika kwa ndugu wa jinsia ya kiume, hasa akimzidi umri mwingine ambaye ni mdogo wake, lakini pengine hata kwa mdogo ikiwa msemaji ni ndugu wa kike anayetaka kuonyesha heshima kwa jinsia ambayo inapewa haki zaidi katika masuala mbalimbali (urithi, ndoa n.k.) kadiri ya utamaduni husika.

Mtoto mdogo na kaka yake huko Haiti.

Mara nyingi mtoto wa kiume wa kwanza ndiye mwenye nafasi ya pekee katika familia, k.mf. katika Biblia.