Hordaland
Hordaland ni moja kati ya Majimbo ya Norwei. Jimbo hili limepakana na Sogn og Fjordane, Buskerud, Telemark na Rogaland. Hordaland ni jimbo la tatu kwa ukubwa baada ya Akershus na Oslo kw idadi ya wakazi. Ngazi ya utawala ya mjini jimboni hapa ipo mjini Bergen. Kabla ya 1972, jiji la Bergen lilikuwa na jimbo lake lenyewe mbali na Hordaland.
Kuhusu jimbo
haririJina la Hordaland
haririHordaland (Kinorse cha Kale: Hǫrðaland) ni jina la dini ya kale ambayo ilifufuliwa upya katika kipindi cha sasa. Elementi ya kwanza ni wingi wa umilikishi wa hǫrðar, jina la kabila la kale la Wagermaniki. Elementi ya mwisho ni land ambayo ina maana ya "nchi" au "kanda".
Hadi 1919 jina la jimbo lilikuwa Søndre Bergenhus amt ambapo ilimaanisha "(upande wa) kusini (mwa) Bergenhus amt". (Bergenhus amt ya kale ilianzishwa mnamo 1662 na iligawanywa mnamo 1763.)
Ngao
haririNgao ilikubali rasmi mnamo tar. 1 Desemba 1961. Zilisanifiwa na Magnus Hardeland, lakini sanifio kuu la awali lilitumiwa kwenye kanda ya Sunnhordland wakati wa karne ya 14t. Mwanzoni mwa karne ya 20, viongozi wa jimboni hapa wakaanza kutumia ngao za zamani ikiwa kama alama ya jimbo kwa mara nyingine tena. Ngao ina rangi nyekundu kwa nyuma ikiwa pamoja na mashoka mawili ya rangi ya dhahabu na taji juu yake.[1]
Historia
haririJimbo la Hordaland lipo zaidi miaka elfu moja iliyopita. Tangu karne ya 7, eneo limetengeneza falme ndogo kadhaa zilizokuwa chini ya Gulating na zilijulikana kama Hordafylke tangu miaka ya 900. Mwanzoni mwa karne ya 16, Norwei ikagawanyika katika len nne. Ambapo Bergenhus len ilikuw ana makao yake makuu mjini Bergen na inazunguka zaidi maeneo ya mjini magharibi na kaskazini mwa Norwei.
Mwaka wa 1662, len ikabadilishwa na kuwa amt. Bergenhus amt inachukua Hordaland, Sogn og Fjordane, Sunnmøre, Troms na Nordland. Mwaka wa 1763, amt ikaganywa katika sehemu za kaskazini na kusini: Nordre Bergenhus amt na Søndre Bergenhus amt. Søndre Bergenhus amt ikabadilishwa jina la Hordaland fylke mnamo 1919.
Jiji la Bergen liliainishwa kama jini-jimbo (byamt) kuanzia 1831-1972. Wakati wa kipindi cha 1915, manispaa ya Årstad ilijumlishwa ndani ya Bergen. Mnamo 1972, manispaa za jirani za Arna, Fana, Laksevåg na Åsane nazo pia zilijumlishwa katika jiji la Bergen. Pia kipindi hichohicho, jiji la Bergen likapoteza hadhi yake ya kuwa jimbo, na kuwa moja kati ya sehemu za Hordaland.
Serikali
haririJimbo (fylke) ni eneo kuu la serikali ya mitaa nchini Norwei. Nchi nzima imegawanyika katika majimbo 19. Jimbo pia ni eneo la uchaguzi, ikiwa na watu kupiga kura kila baada ya miaka minne. Mjini Hordaland, wanachama 57 walichaguliwa kuanzisha baraza la jimbo (Fylkesting). Kuendelea kwa 'Fylkesting ni kazi ya meya wa jimbo (fylkesordførar). Tangu 2003, manispaa za jimbo la Hordaland zimekuwa zikiongozwa na Torill Selsvold Nyborg, meya wa jimbo.
Jimbo pia lina Gavana wa Jimbo (fylkesmann) ambaye ni mwakilishi wa Mfalme na Serikali ya Norwei. Lars Sponheim ni Gavana wa Jimbo la Hordaland.
Manispaa za Hordaland zimegawanyika katika wilaya nne (tingrett): Nordhordland, Sunnhordland, Bergen na Hardanger. Hordaland pia ni sehemu ya wilaya ya Mahakama Rufaa ya Gulating ya mjini Bergen.[2]
- Wilaya za Nordhordland: Askøy, Austevoll, Austrheim, Fedje, Fjell, Fusa, Lindås, Masfjorden, Meland, Modalen, Os, Osterøy, Radøy, Samnanger, Sund, Vaksdal, Voss, Øygarden na Gulen
- Wilaya za Sunnhordland: Bømlo, Etne, Fitjar, Kvinnherad, Stord, Sveio na Tysnes
- Wilaya za Bergen: jiji la Bergen
- Wilaya ya Hardanger: Eidfjord, Granvin, Jondal, Kvam, Odda, Ullensvang na Ulvik
.
Jiografia
haririManispaa
haririManispaa za Hordaland | ||
---|---|---|
Funguo | ||
Marejeo
hariri- ↑ "Hordaland fylke". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-10-04. Iliwekwa mnamo 2008-08-29. (Kinorwei)
- ↑ "Hordaland". Norwegian Bøkmal Wikipedia. Iliwekwa mnamo 2008-08-29. (Kinorwei)
Viungo vya Nje
hariri- County web site Ilihifadhiwa 5 Februari 2005 kwenye Wayback Machine.
- Map of Hordaland Ilihifadhiwa 15 Oktoba 2006 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Norwei bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Hordaland kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |