Hudhi (kwa Kilatini na Kiingereza Auriga) [1]. ni jina la kundinyota kwenye angakaskazi ya Dunia yetu.

Nyota za kundinyota Hudhi (Auriga) katika sehemu yao ya angani
Ramani ya Hudhi - Auriga jinsi inavyoonekana kwa mtazamaji kwenye nusutufe ya kaskazini
Picha kwenye ramani ya Auriga - Hudhi (Uingereza, mnamo 1825)

Mahali pake

Hudhi lipo jirani na makundinyota ya Mapacha (pia Jauza, lat. Gemini) na Ng'ombe (Taurus), ikipakana pia na Farisi (Perseus), Twiga (Camelopardalis) na Pakamwitu (Lynx). Njia Nyeupe inapita katika sehemu ya Hudhi.

Jina

Hudhi ilijulikana kwa jina hili kwa miaka mingi kati ya mabaharia Waswahili walioitumia kupata njia baharini wakati wa usiku.[2]

Jina Hudhi linatokana na ar. al hudhi yaani “dereva wa gari la farasi”. Mitholojia ya Wagiriki wa Kale iliona hapa picha ya shujaa wa kale aliyebuni gari la kuvutwa na farasi nne akibeba mbuzi begani.

Hudhi ni kati ya makundinyota yaliyotajwa tayari na Klaudio Ptolemaio katika karne ya 2 BK. Iko pia katika orodha ya makundinyota 88 ya Umoja wa kimataifa wa astronomia [3]

Nyota

Nyota angavu zaidi ni Ayuki (α Alfa Aurigae) inayojulikana pia kwa jina la kimataifa ya Capella. yenye Mwangaza unaoonekana wa +0.08 mag ikiwa umbali wa Dunia wa miakanuru 42.8 (sawa na 13.1 parsek).

Tanbihi

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Auriga" katika lugha ya Kilatini ni "Aurigae" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Aurigae, nk.
  2. ling. Knappert 1993
  3. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017

Marejeo

  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 75 ff (online hapa kwenye archive.org)
  • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hudhi (kundinyota) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hudhi (kundinyota) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.