Huduma za Vijana
Huduma za vijana, hupelekea ushiriki wa vijana katika shughuli mbalimbali, kitaifa na kijamii. Huduma za vijana kwa upana hutambulika na kudhaminiwa na jamii. Huduma za vijana pia hutoa fursa kwenye maendeleo ya vijana,na kuakisi sauti za vijana.Hii inachukuwa mfumo wa vijana ambapo vijana wanaajiriwa,wanapewa nafasi za uongozi na wanashirikishwa katika shughuli zinazoboresha jamii na wanafunzwa na kuongozwa.
Maana
haririMaana kamili ya huduma za kijamii hutofautiana ingawa uelewa wa vijana hutofautiana kutokana na nchi.Makundi yanayojulikana ya vijana yanaanzia kuanzia miaka 15 - 28.Nchi zilizoendelea hutambua vijana kuanzia miaka 15 - 30.Tofauti ikiwa huduma za vijana ni "masafa marefu" na inategemea mpangilio. Baadhi ya jamii huchukulia huduma ya vijana ni ya masafa marefu kuwa ni kuanzia miezi sita hadi miaka miwili ya utumishi; hata hivyo, muda huu unaweza kutofautiana kulingana na sera ya taifa ya huduma kwa vijana ya kila nchi.
Mipangilio
haririKuna aina mbalimbali za programu za huduma kwa vijana duniani kote.Huduma za kijamii nchini Mexico ni mpango wa huduma za jamii zinazohitajika kwa wanafunzi wote wa chuo kikuu cha Mexico.Wanafunzi lazima watumie masaa 480 za shughuli za kujitolea katika kipindi cha elimu ya miaka minne ya shahada ya kwanza. Lengo ni kujenga ushikamano wa vijana na kuongeza ushirikiano katika maendeleo ya kijamii.[1]Tume ya Taifa ya Vijana nchini Afrika Kusini ni mpango wa kitaifa wa huduma ya vijana na mpango wa kitaifa wa huduma ya vijana unaofadhiliwa na serikali ambao inawashirikisha vijana katika kupambana na kuenea kwa UKIMWI na kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana.[2]Servicio País katika Chile ni mpango wa uteuzi wa ushindani wa huduma za umma kwa wanafunzi wa chuo kikuu na lengo la kupunguza umaskini wa vijijini. Wataalamu waliochaguliwa wanaajiriwa kwenye programu kama vile wanasheria, wahandisi, na wataalamu wa matibabu. Ikiwa walichaguliwa, wahitimu hutumika kwa miezi 13 katika eneo la vijijini. Wao hufanya kazi zao na pia kujenga mahusiano na watu wa ndani. Programu zingine ni pamoja na Servicio País, YouthBuild USA na Mwaka wa Mji.
Marejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-12-20. Iliwekwa mnamo 2022-09-17.
- ↑ National Youth Commission Ilihifadhiwa 28 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine.. Retrieved 4/26/09.