Marekani

nchi katika Amerika Kaskazini
(Elekezwa kutoka USA)

Muungano wa Madola ya Amerika (kwa Kiingereza: United States of America), inajulikana pia kama Marekani (kwa Kiingereza: United States, US, USA au America), ni nchi inayopakana na Kanada na Meksiko katika Amerika ya Kaskazini, mbali ya kuundwa pia na visiwa vya Hawaii.

United States of America
Muungano wa Madola ya Amerika
Bendera ya Marekani Nembo ya Marekani
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: E Pluribus Unum
(kiasili "Moja kutoka wengi")
In God We Trust
(rasmi tangu 1956 "Twamtegemea Mungu")
Wimbo wa taifa: "The Star-Spangled Banner"
("Bendera ya nyota")
Lokeshen ya Marekani
Mji mkuu Washington DC
38°53′ N 77°02′ W
Mji mkubwa nchini New York
Lugha rasmi Kiingereza
hali halisi, si kisheria
Serikali Shirikisho la Jamhuri
Donald Trump
Uhuru
- Matangazo ya uhuru
- Mkataba wa Paris (1783)
Kutoka Uingereza
4 Julai 1776
3 Septemba 1783
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
9,833,517 km² (ya 31)
6.97
Idadi ya watu
 - 2016 kadirio
 - 2010 sensa
 - Msongamano wa watu
 
324,720,797 (ya 3)
309,349,689
35/km² (ya 180)
Fedha Dolar ya Marekani ($) (USD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-5 to -10)
(UTC-4 to -10)
Intaneti TLD .us .gov .edu .mil .um
Kodi ya simu +1Mji mkuu wa Marekani ni Washington DC.

Eneo

Marekani bara

 
Picha kutoka angani ikionyesha majimbo 48 ya Marekani yanayopakana

Eneo la Marekani lina ukubwa wa kilometa mraba 9,826,675 na liko hasa katika bara la Amerika Kaskazini kati ya Kanada upande wa kaskazini na Meksiko upande wa kusini.

Marekani imeunganisha upana wote wa bara kutoka Bahari ya Atlantiki hadi Pasifiki, ikigawanywa kwa majimbo 48 yanayojitawala.

Eneo hilo lagawiwa katikati na mto mkubwa Mississippi unaoanza mpakani kwa Kanada na kuishia katika Ghuba ya Meksiko.

Alaska

Jimbo la Alaska liko pia kwenye bara la Amerika Kaskazini upande wa kaskazini kutoka Kanada kuelekea Urusi, lakini halipakani na jimbo lolote la Marekani.

Hawaii

Funguvisiwa ya Hawaii ni jimbo la visiwani katika bahari ya Pasifiki. Ni jimbo la 50 na la mwisho mpaka sasa.

Visiwa vya ng'ambo vya Marekani

Maeneo ya ng'ambo ya Marekani ni visiwa kadhaa ambavyo ni maeneo ya Kimarekani ingawa si sehemu ya jimbo lolote. Zamani yalikuwa kama makoloni hata kama Marekani ilidai kutokuwa na ukoloni. Siku hizi maeneo haya yamepata viwango mbalimbali vya kujitawala. Kwa kawaida maeneo haya huchagua pia wawakilishi kwa ajili ya bunge la Marekani lakini wawakilishi hao si wabunge wa kawaida, bali wana haki ya kusema na kushauri tu bila haki ya kupiga kura.

Visiwa muhimu kati ya hivyo ni kama ifuatavyo:

Milima

Baadhi ya milima ya Marekani ni: A B C D E F G H I J K L M N O P Q R S T U V W X Y Z

A
B
C
D
E
F
G
H
I
J
K
L
M
N
O
P
Q
R
S
T
U
V
W
X
Y
Z

Mito

Baadhi ya mito ya Marekani ni:

Historia

 
Uenezi wa nchi hatua kwa hatua.

Nchi ilianza kama mkusanyiko wa makoloni ya Uingereza kwenye pwani ya mashariki ya Amerika ya Kaskazini tangu karne ya 17. Walowezi kutoka Uingereza walijipatia ardhi wakipigana na wenyeji Waindio.

Katika vita ya uhuru wa Marekani makoloni yalipata uhuru wao uliotangazwa mwaka 1776 na kukubaliwa na Uingereza baada ya vita mwaka 1783.

Baadaye Marekani ilipanua eneo lake hadi bahari ya Pasifiki ikatwaa ardhi ya Maindio wazalendo, ikapokea wahamiaji wengi kutoka nchi zote za Ulaya pamoja na watumwa walioletwa kutoka Afrika.

Tangu karne ya 19 wahamiaji walifika pia kutoka Asia, hasa China na Japani.

Katika vita na Hispania na Meksiko Marekani ilipanua eneo lake kwenda kusini.

Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani ilipigwa kuanzia 1861 hadi 1865 kati ya majimbo ya kusini na majimbo ya kaskazini nchini Marekani. Sababu mojawapo muhimu ya vita ilikuwa suala la utumwa. Majimbo ya kaskazini yaliwahi kupiga utumwa marufuku lakini majimbo ya kusini yaliendelea na sheria zilizoruhusu utumwa na matajiri wengi wa kusini walitegemea kazi ya watumwa. Mafarakano yalianza kuhusu swali kama madola mapya yaliyoanzishwa katika Amerika Kaskazini na kujiunga Muungano yangeruhusiwa kukubali utumwa au la. 1861 madola ya kusini-mashariki yalitangaza kuondoka katika Muungano na kuanzisha "Shirikisho la Madola ya Amerika". Vita ilianza na kudumu miaka minne na watu 650.000 walikufa, lakini mwishoni kaskazini ilishinda.

 
100 Dollars

Watu

Nchi ina wakazi zaidi ya milioni 320, na ina mchanganyiko mkubwa kuliko nyingine zote duniani.

Lugha

Ingawa Muungano hauna lugha rasmi, majimbo yake 32 yanaipa hadhi hiyo lugha ya Kiingereza, iliyo lugha ya kwanza kwa asilimia 80 ya wakazi.

Wakazi wengine wanatumia lugha nyingine nyingi, hasa kulingana na nchi ya asili ya ukoo wao. Kati ya lugha hizo, inaongoza kwa mbali ile ya Kihispania (12%).

Dini

Nchini dini zote zina uhuru mkubwa, tena kwa asilimia 59 ya wakazi dini ina umuhimu wa hali ya juu, tofauti na nchi tajiri nyingine duniani.

Asilimia 70.6 hivi ya wakazi wanafuata Ukristo katika mojawapo ya madhehebu yake, hasa ya Uprotestanti (46.5%), ingawa ile kubwa zaidi ni Kanisa Katoliki (20.8%).

Dini nyingine zina asilimia 4.7, na kati yake inaongoza ile ya Uyahudi (1.9%), ikifuatwa na Uislamu (0.9%).

Watu maarufu

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
  • Official U.S. Government Web Portal Gateway to government sites
  • House Official site of the United States House of Representatives
  • Senate Official site of the United States Senate
  • White House Official site of the President of the United States
  • [[[:Kigezo:SCOTUS URL]] Supreme Court] Official site of the Supreme Court of the United States
Historia
Ramani
Vingine
  Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Marekani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Majimbo na maeneo ya Marekani
Majimbo ya Marekani
AlabamaAlaskaArizonaArkansasCaliforniaColoradoConnecticutDelawareFloridaGeorgiaHawaiiIdahoIllinoisIndianaIowaKansasKentuckyLouisianaMaineMarylandMassachusettsMichiganMinnesotaMississippiMissouriMontanaNebraskaNevadaNew HampshireNew JerseyNew MexicoNew YorkNorth CarolinaNorth DakotaOhioOklahomaOregonPennsylvaniaRhode IslandSouth CarolinaSouth DakotaTennesseeTexasUtahVermontVirginiaWashingtonWest VirginiaWisconsinWyoming
Mkoa wa Mji Mkuu
Mkoa wa Columbia (Washington D.C.)
Visiwa vya ng'ambo
Katika Pasifiki: Samoa ya MarekaniVisiwa vya Mariana ya KaskaziniGuamKatika Karibi: Puerto RicoVisiwa vya Virgin vya MarekaniVisiwa vidogo sana vya Pasifiki:Kisiwa cha HowlandKisiwa cha Jarvis Atolli ya JohnstonKingman ReefAtolli ya MidwayKisiwa cha BakerAtolli ya PalmyraKisiwa cha WakeKisiwa kidogo cha Karibi: Kisiwa cha Navassa