I Don't Want to Miss a Thing
"I Don't Want to Miss a Thing" ni wimbo wa aina ya power ballad ulioimbwa na bendi ya muziki wa rock kutoka nchini Marekani Aerosmith. Wimbo huu umepata kuonekana kama kibwagizo cha filamu ya Armageddon na kuingia nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard Hot 100 (ya kwanza kwa bendi kuingia nafasi ya kwanza baada ya miaka 28 ya pamoja).
“I Don't Want to Miss a Thing” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Single ya Aerosmith kutoka katika albamu ya Armageddon Soundtrack | |||||
B-side | "Animal Crackers"/"Taste of India" | ||||
Imetolewa | 12 Septemba 1998 | ||||
Muundo | Cassette, CD | ||||
Imerekodiwa | 1997 | ||||
Aina | Rock, Soft rock, Blues | ||||
Urefu | 4:58 (Album Version) 4:28 (Single Version) | ||||
Studio | Columbia/Hollywood/Epic | ||||
Mtunzi | Diane Warren | ||||
Mtayarishaji | Mark Wright | ||||
Certification | Gold (RIAA) | ||||
Mwenendo wa single za Aerosmith | |||||
|
Wimbo uliendelea kukaa kwenye chati kwa takriban majuma manne kuanzia tar. 5 Septemba hadi 26 Septemba 1998, ina watambulisha Aerosmith kwenye washabiki wa kizazi kipya. Wimbo pia ulikaa nafasi ya kwanza kwa majuma kadhaa kwenye nchi mbalimbali. Wimbo ulitamba vya kutosha kwenye chati za Uingereza, kwa kushika nafasi ya nne mnamo mwezi wa Novemba katika mwaka wa 1998 na kuufanya kuwa wimbo pekee wa Aerosmith kushika nafasi ya juu nchin Uingereza hadi leo hii.
"I Don't Want to Miss a Thing" ulitungwa na Diane Warren[1]. Alieleza kwenye albamu yake ya kompilesheni Diane Warren Presents Love Songs kwamba awali wimbo huu aliutunga kwa ajili ya Celine Dion.
Chati
hariri
Nafasi ilizoshikahariri
|
Chati za mwisho wa mwakahariri
|
Orodha ya nyimbo
haririCD Single
- "I Don't Want to Miss a Thing" (4:58)
- "I Don't Want to Miss a Thing" [Rock Mix] (4:58)
- "Taste of India" [Rock Remix] (5:52)
- "Animal Crackers" (2:36)
Wimbo umeonekana kwenye toleo la albamu ka Kiargentina Nine Lives. Pia umeonekana kwenye toleo la Kijapani la Just Push Play.
CD Single 2
- "I Don't Want To Miss A Thing [Pop Mix](4:58)
- "Pink [Live] (3:45)
- "Crash (4:26)
Marejeo
hariri- ↑ http://www.imdb.com/title/tt0120591/soundtrack
- ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 2.6 2.7 Euro Peakpositions
- ↑ 3.0 3.1 ultratop.be - Aerosmith - I Don't Want To Miss A Thing
- ↑ "Billboard Top 100 - 1998". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-03-09. Iliwekwa mnamo 2010-08-28.