Ijuganyondo
Ijuganyondo ni kata ya Manisipaa ya Bukoba katika Mkoa wa Kagera, Tanzania, yenye postikodi namba 35105 [1].
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 2,670 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 2,591 waishio humo.[3]
Kata ya Ijuganyondo imegawanyika katika sehemu mbili yaani Ijuganyondo A na Ijuganyondo B. Pia ina mitaa kama vile Kahembe, Bulungi, Omukatoma, Ruti, Ibura, Magoti.
Ndani ya kata ya Ijuganyondo kuna shule mbili za sekondari yaani Ijuganyondo Secondary School na Kemebos Primary and Secondary School (ya binafsi); pia kuna shule tatu za msingi ambazo ni Ibura Primary School, Kituo Shikizi Ruti, na Mshemba Trinity Primary School (ya binafsi)
Kata ya Ijuganyondo ina Uwanja wa Michezo pale Ruti.
Marejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
- ↑ https://www.nbs.go.tz, uk 172
- ↑ Sensa ya 2012, Kagera - Bukoba Municipal Council
Kata za Wilaya ya Bukoba Mjini - Mkoa wa Kagera - Tanzania | ||
---|---|---|
Bakoba | Bilele | Buhembe | Hamugembe | Ijuganyondo | Kagondo | Kahororo | Kashai | Kibeta | Kitendaguro | Miembeni | Nshambya | Nyanga | Rwamishenye |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ijuganyondo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |