Ekolojia

(Elekezwa kutoka Ikolojia)

Ekolojia (gir. οἶκος oikos "nyumba" + -λογία logia "elimu ya..") ni tawi la biolojia inayoangalia viumbehai na mazingira yao, kama ni hali asilia au viumbehai wengine.

Kwa hiyo ukiuliza jinsi gani samaki wanahusiana na samaki na wanyama wengine na binadamu pamoja na mimea na hali ya maji wanamoishi unauliza maswali kuhusu ekolojia yao.

Wataalamu wa ekolojia huchungulia kila kitu kuanzia bakteria ndogo katika myeyusho wa kuwalisha hadi athira ya msitu wa mvua kwa halihewa ya dunia.

Ekolojia inalenga kuelewa jinsi gani pande mbalimbali za uhai duniani zinahusiana na mazingira yao. Kila spishi ya viumbehai inategemea makazi maalumu kwa kudumisha maisha yake. Hapo ekolojia inachungulia pia athira ya mabadiliko yanayosababishwa na binadamu kwa makazi haya na ekolojia yao.

Kwa mfano matumizi ya madawa ya kuua wadudu katika kilimo yanaweza kubadilisha ekolojia ya makazi kwa nyuki; kupotea kwa nyuki katika eneo kunaathiri pia kustawi wa mimea inayotegemea nyuki kwa kuzalisha matunda yao.

Kwa hiyo ekolojia ni elimu ya msingi kwa kutambua uharibifu wa mazingira na kutambua hatua muhimu ya kuhifadhi mazingira.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ekolojia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.