Tunda

(Elekezwa kutoka Matunda)

Matunda ni sehemu za mimea zilizo na mbegu ndani yao.

Fyulisi kama mfano wa tunda:
katikati iko kokwa yenye mbegu;
sehemu nene la nyama ya tunda ambayo ni sehemu ya kuliwa
ganda la nje kabisa linafunika tunda lote kama ngozi.
Sahani ya matunda

Kwa lugha ya biolojia ni ovari ya ua iliyoiva. Ovulo au chembekike ndani ya ovari zinakuwa mpaka kuwa mbegu. Kwa hivyo hata kokwa, matumba ya maharagwe, nyanya na matango ni matunda kwa kibiolojia. Lakini kwa lugha ya kila siku tunda lina nyama tamu au chungu. Nyanya na matango huitwa mboga kwa kawaida.

Ukuta wa ovari huunda ganda la tunda na nyama pia kama iko. Kama nyama hii ina lishe kwa binadamu na ladha ya kupendeza basi ni tunda la kuliwa.

Matunda mengi yana maji ndani yao pamoja na sukari asilia. Asilimia kubwa ya tunda ni nyuzi za vitembwe. Ina kiasi kikubwa cha vitamini na madini kama chuma. Kwa kawaida matunda hayana protini na mafuta mengi isipokuwa matunda ya pekee kama maparachichi.

Picha hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tunda kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.