Wilaya ya Ilala

(Elekezwa kutoka Ilala)

Coordinates: 6°49′26″S 39°14′56″E / 6.824°S 39.249°E / -6.824; 39.249

Wilaya ya Ilala ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania yenye postikadi namba 12000[1]. Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 634,924. Eneo lake ni km² 273.

Mandhari ya sehemu ya Ilala.
Mtaa wa Samora ni kati ya barabara kuu za kitovu cha jiji.

Ilala yenyewe inahesabiwa kama manispaa ya Ilala ndani ya jiji la Dar es Salaam. Inajumlisha kitovu cha kihistoria cha Dar es Salaam ambako kuna ofisi nyingi za serikali pamoja na makampuni makubwa na maduka. Nafasi ya kitovu chenyewe ni Sanamu ya Askari; mitaa mingine maarufu ni Kariakoo, Buguruni, Kivukoni na kando yake iko Pugu.

Marejeo Edit

  Kata za Wilaya ya Ilala - Tanzania  

BuguruniChanikaGerezaniGongo la MbotoIlalaJangwaniKariakooKimangaKinyereziKipawaKisutuKitundaKivukoniKiwalaniMajoheMchafukogeMchikichiniMsongolaPuguSegereaTabataUkongaUpanga MagharibiUpanga MasharikiVingunguti