6°49′26″S 39°14′56″E / 6.824°S 39.249°E / -6.824; 39.249

Mandhari ya sehemu ya Ilala.
Mtaa wa Samora ni kati ya barabara kuu za kitovu cha jiji.

Wilaya ya Ilala (Dar es Salaam City) ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania, yenye postikadi namba 12000. Upande wa kaskazini na kaskazini-mashariki imepakana na wilaya ya Kinondoni na ya Ubungo, upande wa magharibi imepakana na Wilaya ya Ubungo, kusini imepakana na Wilaya ya Temeke.

Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 634,924. Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 1,649,912 [1].

Eneo lake ni km² 273, likijumlisha kitovu cha kihistoria cha jiji la Dar es Salaam ambako kuna ofisi nyingi za serikali pamoja na kampuni kubwa na maduka. Nafasi ya kitovu chenyewe ni Sanamu ya Askari; mitaa mingine maarufu ni Kariakoo, Buguruni, Kivukoni na kando yake iko Pugu.

Marejeo

hariri
  Kata za Wilaya ya Ilala - Tanzania  

Bonyokwa | Buguruni | Buyuni | Chanika | Gerezani | Gongolamboto | Ilala | Jangwani | Kariakoo | Kimanga | Kinyerezi | Kipawa | Kipunguni | Kisukuru | Kisutu | Kitunda | Kivukoni | Kivule | Kiwalani | Liwiti | Majohe | Mchafukoge | Mchikichini | Minazi Mirefu | Mnyamani | Msongola | Mzinga | Pugu | Pugu Station | Segerea | Tabata | Ukonga | Upanga Magharibi | Upanga Mashariki | Vingunguti | Zingiziwa