Injini ya dizeli

(Elekezwa kutoka Injini za dizeli)

Injini ya dizeli ni injini ya mwako ndani ambamo kuwaka kwa mafuta husababishwa na joto la juu linalotokana na kugandamiza hewa ndani ya silinda zake. Hii ni tofauti na injini zinazowasha mchanganyiko wa mafuta na hewa kwa njia ya heche za umeme, kama vile injini ya petroli au injini ya gesi (gesi asilia au gesi ya LPG). Injini ya dizeli ilibuniwa na mhandisi Mjerumani Rudolf Diesel katika karne ya 19.

Injini ya dizeli ya Mercedes Benz ( silinda 6)
Filamu kuhusu maendeleo ya ijini za diseli kutoka kampuni ya Shell

Injini ya diseli inahitaji kutengeneza shinikizo kali ndani yake hivyo ni imara na nzito zaidi kuliko injini ya petroli. Hapo awali ilitumika kama mbadala wa injini za mvuke zilizosimama . Tangu miaka ya 1910, zilitumika pia katika manowari na meli. Iliendelea kutumika katika vichwa vya trenimabasimalorimatrekta na majenereta ya kuzalisha umeme. Katika miaka ya nyuma mahandisi walifaulu kutengeneza pia injini ndogo za diseli zinazotumiwa katika magari madogo. 

Tangu miaka ya 1970, matumizi ya injini za dizeli katika magari makubwa ya barabarani na nje ya barabara nchini Marekani yameongezeka. Kulingana na Konrad Reif (2012), nusu ya magari madogo katika Umoja wa Ulaya ni magari ya dizeli.

Injini kubwa zaidi za dizeli zinazotumiwa duniani zina silinda 14 zinazotumiwa kwenye meli kubwa.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Hataza

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.