Interscope Records

(Elekezwa kutoka Interscope)

Interscope Records ni studio ya muziki ya Kimarekani, inayomilikiwa na studio ya Universal Music Group, na inafanyakazi kama moja kati ya studio tatu za UMG - Interscope-Geffen-A&M. Studio ilianzishwa mnamo mwaka wa 1990.

Interscope Records
Shina la studio Universal Music Group
Imeanzishwa 1990
Mwanzilishi Jimmy Iovine
Ted Field
Tom Whalley
Ilivyo sasa Inafanya kazi
Usambazaji wa studio Interscope-Geffen-A&M (US)
Polydor Records (UK)
Aina za muziki Mbalimbali
Nchi Marekani
Mahala Santa Monica, California
Tovuti http://interscope.com/

Historia

hariri

Hapo awali

hariri

Interscope ilianzishwa mnamo mwaka wa 1990 na Bw. Jimmy Iovine, Ted Field, na Tom Whalley kwa msaada wa kifedha uliotolewa na studio ya Atlantic Records (ambayo ilikuwa inachukua asilimia 50 ya mapato ya studio).

Wakati studio inaanza kazi zake, mwanzoni zilikuwa zikisambazwa na Atlantic Records ikiwa chini ya East West Records ya Amerika.

Studio kwa mara ya kwanza ilitoa kazi ya rapa wa Kilatini-Gerardo, ambaye alishinda tano bora, kwa kibao chake mahili cha "Rico Suave" kunako mwaka wa 1991.

Mafanikio mengine ya awali na baadaye, ni pale walipotoa albamu ya kwanza ya Marky Mark and the Funky Bunch, ambayo ilikwenda moja kwa moja katika platinam za mwanzoni mwa mwaka wa 1992. Wakati wa kipindi hicho, Interscope pia ikaingia mkataba na baadhi ya wasanii wa rap na hip hop kama vile Tupac Shakur, Primus, No Doubt na Nine Inch Nails."[1]

Wasanii wa Interscope

hariri

Studio ambazo ziko chini ya Interscope

hariri
Makala kuu ya: Universal Music Group

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. Ice Cube – Child Support Lyrics Ilihifadhiwa 6 Julai 2008 kwenye Wayback Machine.. LyricsDomain. Accessed 25 Machi 2008.

Viungo vya nje

hariri