Interscope Records
Interscope Records ni studio ya muziki ya Kimarekani, inayomilikiwa na studio ya Universal Music Group, na inafanyakazi kama moja kati ya studio tatu za UMG - Interscope-Geffen-A&M. Studio ilianzishwa mnamo mwaka wa 1990.
Interscope Records | |
---|---|
Shina la studio | Universal Music Group |
Imeanzishwa | 1990 |
Mwanzilishi | Jimmy Iovine Ted Field Tom Whalley |
Ilivyo sasa | Inafanya kazi |
Usambazaji wa studio | Interscope-Geffen-A&M (US) Polydor Records (UK) |
Aina za muziki | Mbalimbali |
Nchi | Marekani |
Mahala | Santa Monica, California |
Tovuti | http://interscope.com/ |
Historia
haririHapo awali
haririInterscope ilianzishwa mnamo mwaka wa 1990 na Bw. Jimmy Iovine, Ted Field, na Tom Whalley kwa msaada wa kifedha uliotolewa na studio ya Atlantic Records (ambayo ilikuwa inachukua asilimia 50 ya mapato ya studio).
Wakati studio inaanza kazi zake, mwanzoni zilikuwa zikisambazwa na Atlantic Records ikiwa chini ya East West Records ya Amerika.
Studio kwa mara ya kwanza ilitoa kazi ya rapa wa Kilatini-Gerardo, ambaye alishinda tano bora, kwa kibao chake mahili cha "Rico Suave" kunako mwaka wa 1991.
Mafanikio mengine ya awali na baadaye, ni pale walipotoa albamu ya kwanza ya Marky Mark and the Funky Bunch, ambayo ilikwenda moja kwa moja katika platinam za mwanzoni mwa mwaka wa 1992. Wakati wa kipindi hicho, Interscope pia ikaingia mkataba na baadhi ya wasanii wa rap na hip hop kama vile Tupac Shakur, Primus, No Doubt na Nine Inch Nails."[1]
Wasanii wa Interscope
haririStudio ambazo ziko chini ya Interscope
hariri- A&M Records Tovuti Rasmi - A&M Records, Tovuti Rasmi (moja ya sehemu ya Universal Music Group)
- A&M/Octone Records Tovuti Rasmi Archived 26 Juni 2012 at the Wayback Machine. - A&M/Octone Records, Tovuti Rasmi
- Cherrytree Records Tovuti Rasmi - Cherrytree Records, Tovuti Rasmi
- Aftermath Records Tovuti Rasmi - Aftermath Records, Tovuti Rasmi
- G-Unit Records Tovuti Rasmi - G-Unit Records, Tovuti Rasmi
- Mosley Music Group Tovuti Rasmi Archived 2 Julai 2010 at the Wayback Machine. - Mosley Music Group, Tovuti Rasmi
- Shady Records Tovuti Rasmi Archived 17 Septemba 2020 at the Wayback Machine. - Shady Records, Tovuti Rasmi
- Tennman Records Tovuti Rasmi - Tennman Records, Tovuti Rasmi
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ Ice Cube – Child Support Lyrics Archived 6 Julai 2008 at the Wayback Machine.. LyricsDomain. Accessed 25 Machi 2008.