Islamabad
Islamabad (Kiurdu: اسلام آباد) ni mji mkuu wa Pakistan. Iko katika kaskazini-mashariki ya nchi mguuni wa milima ya Himalaya na kijiografia sehemu ya Punjab ingawa kisiasa eneo lake limetengwa kutoka jimbo la Punjab kwa ajili ya mji mkuu.
Msikiti ya Shah Faisal mjini Islamabad (Pakistan) | |
Mkoa | Eneo la mji mkuu Islamabad (Islamabad Capital Territory) |
Anwani ya kijiografia | Latitudo: 33°40′N - Longitudo: 73°10′E. |
Kimo | 457 – 610 m juu ya UB |
Eneo | 906 km² |
Wakazi | 1,019,000 (1999) |
Msongamano wa watu | watu 1,123 kwa km² |
Simu | +92 (nchi), 51 (mji) |
Mahali | |
Islamabad ni mji mpya. Azimio la kuujenga lilichakuliwa na rais Ayyub Khan mwanzo wa miaka ya 1960 aliyeamua kuhamisha mji mkuu kutoka Karachi kwenda kaskazini. Mji jirani wa Rawalpindi ukawa mji mkuu wa muda hadi kumalizika kwa Islamabad.
Mji ulipangwa shambani kwa kufuata muundo wa miraba. Mpangilio umekuwa na kanda nane kama vile kanda la balozi, la biashara, la elimu (shule na vyuo), la viwanda na kadhalika. Kila kanda limepewa maeneo mapana ya bustani, msikiti na soko.
Msikiti wa Shah Faisal ni msikiti kubwa duniani.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Islamabad kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |