Jacqueline Mutere

mwanzilishi na mkurugenzi wa Grace Agenda

Jacqueline Mutere ni mwanaharakati wa haki za wanawake wa Kenya, na mwanzilishi wa Grace Agenda linalo hushughulika na kutoa usaidizi na ushauri kwa waathiriwa wa ubakaji nchini Kenya. Mutere pia ni mwanachama wa shirika la National Victims and Survivors Network, shirika ambalo linalenga kuendeleza ajenda ya fidia ya Tume ya Ukweli, Haki na Maridhiano (TJRC).

Harakati

hariri

Katika ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007-2008 nchini Kenya kutokana na uchaguzi wenye utata, watu 1,000 waliuawa na takriban wanawake na wasichana 900 walifanyiwa ukatili wa kijinsia . Mutere vile vile alibakwa na kupachikwa mimba na jirani. Alitaka kutoa mimba, lakini kwa sababu sheria imekataza nchini Kenya, akajifungua binti, Princess. Uzoefu wake mwenyewe na uthabiti ulimtia motisha kusaidia waathirika wengine na watoto wao kwa kuanzisha Grace Agenda.[1]

Mutere alianzisha Grace Agenda mnamo mwaka 2010 ili kusaidia watoto wa waathiriwa wa ubakaji kutoka kwenye wimbi hilo la ghasia za kikabila . Muda mfupi baada ya kuunda msingi huo, Mutere aligundua kuwa akina mama wengi wa watoto hawa pia walihitaji mahali salama kwa kujadili kiwewe chao, na kwamba kwa kutoa njia hiyo, akina mama wachache wangepitisha kiwewe chao kwa watoto wao . Kutokana na machafuko yaliyokuwepo wakati wa vurugu hizo, ugumu wa kuwatambua washambuliaji, wengi wao wakiwa polisi, na wahanga wengi kushindwa kujitokeza hadharani, shirika hili lilijitolea kuzungumza kwa ajili ya walionusurika. Shirika lake huwasaidia waathiriwa kwa kutuma manusura kama waangalizi wa kuwasindikiza katika ziara hizo za vituo vya afya baada ya kudhulumiwa..[2] Mutere anasema, "Kundi hili ni muhimu sana katika kuhamisha michakato inayowasaidia walionusurika; wawakilishi wanaripoti wao kwa wao, ikiwa ni pamoja na serikali, ili wajue nini cha kutarajia."[1]

Harakati za Janga la Korona

hariri

Wakati wa janga la ugonjwa wa korona, kazi ya Mutere kama mtetezi wa haki za wanawake ilifanywa kuwa ngumu zaidi kwa hofu kwamba wanawake wanaotembelea vituo vya afya kwa sababu ya unyanyasaji wa kijinsia au unyanyasaji wa majumbani wangejaribiwa na kutengwa kwa lazima, na kwa shida za kiuchumi zinazoletwa na jamii. Mutere anaendelea kutetea na kusaidia waathiriwa katika kesi mpya, kama vile kutafuta haki kwa kutoa ushahidi katika vikao vya mahakama, kutembelea hospitali, na kuhudhuria ushauri nasaha, miongoni mwa masuala mengine ya matibabu ya baada ya kushambuliwa kwa waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia.[2]

Mutere pia anaangazia kuishinikiza serikali ya Kenya kufuata ahadi yake ya kusambaza fidia ya zaidi ya dola milioni 100 za Marekani kwa walionusurika kwa ubakaji wakati wa machafuko ya 2007-2008. Juhudi hizi zilijumuisha maandamano ya amani kuwasilisha ombi kwa seneti ya Kenya kuwakumbusha wanachama wake kuhusu ahadi walizotoa kwa walionusurika ubakaji. Kikundi pia kinatetea utu wa waathirika.

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 Affairs, Berkley Center for Religion, Peace and World. "A Discussion with Jacqueline Mutere, Founder and Director of Grace Agenda". berkleycenter.georgetown.edu (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-07-28.{{cite web}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  2. 2.0 2.1 "Stand up for Human Rights". www.standup4humanrights.org (kwa Kiingereza). 2020. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Desemba 2020. Iliwekwa mnamo 2021-03-29.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)