Jacques Cartier (31 Desemba 14911 Septemba 1557) alikuwa baharia na mpelelezi kutoka nchini Ufaransa aliyefanya safari tatu kwenda Amerika ya Kaskazini. Safari za Cartier zilikuwa msingi wa koloni ya Ufaransa katika eneo la Kanada ya leo.

Cartier alikuwa mwenyeji wa mji wa Saint-Malo katika kaskazini-magharibi ya Ufaransa iliyokuwa bandari ya wavuvi wenye uzoefu wa kuwa na safari ndefu baharini. 1534 alifanya safari yake ya kwanza ya kwenda Amerika Kaskazini kwa amri ya mfalme François I aliyemwagiza "kupeleleza visiwa na nchi zinaposemekana kuwa na dhahabu na vitu vingine vyenye thamani". Wakati ule taarifa juu ya dhahabu na fedha za Amerika zilipatikana tayari kupitia Wahispania waliowahi kuvamia sehemu kubwa za Amerika ya Kati na Kusini.

Cartier alifika kwenye pwani za Newfoundland na Quebec za leo akakutana na makabila ya Maindio wenyeji akasimamisha msalaba kama angazo ya kwamba alidai eneo kwa ajili ya mfalme wa Ufaransa. Alirudi mara mbili.

Cartier alipeleleza kisiwa cha Newfoundland, kisiwa cha Prince Edward Island, mto Saint Lawrence na mahali pa Montreal ya baadaye alipokuta kijiji kikubwa sana ya Maindio.

Kwenye safari yake ya tatu alikwenda na walowezi wa kwanza Wafaransa waliojaribu kuanzisha makazi ya kwanza ya Wafaransa katika Kanada lakini hawakuelewana na wenyeji wakapaswa kurudi.

Baada ya Cartier Wafaransa waliendelea kutembelea pwani za Kanada hadi 1608 walipounda makazi ya kwanza ya kudumu yaliyokuwa baadaye mji wa Quebec.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jacques Cartier kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.