Jairam Shivji (1792–1866) alikuwa mfanyabiashara na mwanabenki kutoka wilaya ya Kutch, nchini India.

Shivji alikuwa anaendesha shughuli zake za kiuchumi kutoka kisiwa cha Zanzibar na nchini Muskat na aliwahi kuwa mtu tajiri zaidi Afrika Mashariki wakati alipokuwa hai [1] [2] [3]

Historia hariri

Jairam Shivji alizaliwa nchini India, mwaka 1792, katika familia ya Uhindu wa tabaka la Bhatia huko mjini Mundra, Wilaya ya Kutch. Baba yake Shivji Topan alikuwa mfanyabiashara kutoka Muscat, na alikuwa ameandamana na Sultani wa Oman kwenye msafara wa kudumisha ushawishi wake katika Afrika Mashariki mnamo 1785 pamoja na mfanyabiashara mwingine aliyeitwa Vansanji Haridas Bhimani.

Katika kipindi cha biashara kuongezeka wa kasi na mataifa ya magharibi, Usultani wa Omani waliweka kandarasi na mamlaka mbalimbali na makampuni kukusanya ushuru wa forodha katika maeneo mbalimbali. Baba yake Jairam, Shivji Topan, alipata kandarasi ya kukusanya ushuru wa forodha wa kisiwa cha Zanzibar mwaka 1819.

Shivji alisafiri kisiwa cha Zanzibar and alijiunga na baba yake na baba mdogo wake, Madhavji Topan kama mwanafunzi na kusaidia katika biashara ya baba.

Baada kuirithi biashara ya baba yake, aliunganisha mikusanyiko maalum wa Usultani wa Omani na kudhibiti biashara kwenye ukanda wa pwani wenye urefu wa maili elfu moja. Makao makuu ya ofisi yake ilikuwa kisiwani Zanzibar na watoza ushuru wa eneo hilo walikuwa wanaitwa Kutchi Banias (watu waliotoka wilaya ya Kutch, nchini India).

Walijulikana pia kama Wahindi wa Bandari au Baniani Forodha . Baada ya hapa alijulikana kwa jina la 'Jiram Sewji'.

Sultan Sayyid Said alikuwa alipiga marufuku kuchinja ng'ombe karibu na nyumba yake wakati wa Eid al-Fitr, ili kuheshimu imani ya kidini ya Shivji, ambaye alikuwa Mhindu.

Kifo na urithi hariri

Shivji alifariki tarehe 25 Agosti 1866. Alikuja kujulikana kwa jina la Mswahili na familia yake ilichukua jina la Swali. Barabara karibu na nyumba yake huko mjini Mundra ilijulikana kama Swali Sheri.

Tanbihi hariri

  1. Goswami, Chhaya R. (2006). "Professor J.C. Jha Memorial Prize Essay: The ivory trade at Zanzibar and the role of Kutchis". Proceedings of the Indian History Congress 67: 921–935. ISSN 2249-1937.  Unknown parameter |url-access= ignored (help)
  2. McDow, Thomas F. (2018). Buying Time: Debt and Mobility in the Western Indian Ocean (kwa Kiingereza). Ohio University Press. uk. 89. ISBN 978-0-8214-4609-6. 
  3. Mehta, Makrand (2001). "Gujarati Business Communities in East African Diaspora: Major Historical Trends". Economic and Political Weekly 36 (20): 1738–1747. ISSN 0012-9976.