Uhindu
Uhindu (kwa Kisanskrit: हिन्दू धर्म: Hindū Dharma; pia सनातन धर्म Sanātana Dharma) ni dini kubwa yenye asili katika Bara Hindi.
Ikiwa na wafuasi milioni 900 ni dini ya tatu baada ya Ukristo na Uislamu kwa wingi wa waumini.
Nchi zenye Wahindu
haririKatika nchi za India, Nepal na Morisi na kwenye kisiwa cha Bali (Indonesia) wakazi wengi hufuata aina mojawapo ya Uhindu.
Vikundi vikubwa viko pia:
- Bangladesh (11 millioni),
- Myanmar (7.1 millioni),
- Pakistan (3.3 millioni),
- Sri Lanka (2.5 millioni),
- Marekani (2.0 millioni)
- Afrika Kusini (1.2 millioni),
- Uingereza (1.2 millioni),
- Malaysia (1.1 millioni),
- Kanada (0.7 millioni),
- Fiji (0.5 millioni),
- Trinidad na Tobago (0.5 millioni),
- Guyana (0.4 millioni),
- Uholanzi (0.4 millioni),
- Singapur (0.3 millioni)
- Surinam (0.2 millioni).
Jina
haririNeno Hindu linatokana na lugha ya Kisanskrit ambapo Sindhu ni jina la kale la mto Indus uliopo kwenye sehemu ya magharibi kaskazini ya Bara Hindi. "Hindu" imepatikana mara ya kwanza wakati wa karne ya 6 KK katika andishi la mfalme Darius I kwa maana ya "watu wa ng'ambo ya mto Indus (Kisanskrit: Sindhu).[1] Hapa "Sindhu / Hindu" haina maana ya kidini bali ya kijiografia pekee.
Katika Kiajemi neno "Hindu" linamaanisha wakazi wa Uhindi pamoja na wafuasi wa dini kubwa ya nchi hiyo. Mnamo karne ya 11 milki iliundwa na Waajemi katika Bara Hindi iliyoitwa "Hindustan" na mji mkuu ulikuwa Lahore[2].
Baadaye Waingereza walipokea jina hilo kutoka Kiajemi, wakilitumia kwanza kwa nchi na baadaye hasa kwa wafuasi wa dini zisizo za Kiislamu, Kiyahudi wala Kikristo. Jina Hinduism (iliyoandikwa mwanzoni Hindooism) lilikuwa kawaida tangu karne ya 18 kwa kutaja falsafa na dini zenye asili ya India.[3]
Marejeo
hariri- ↑ Flood, Gavin D. (1996), An Introduction to Hinduism, Cambridge University Press, uk. 6
- ↑ J. T. P. de Bruijn, makala HINDU kwa Encyclopædia Iranica Vol. XII, Fasc. 3, pp. 311-312, inapatikana online kwa http://www.iranicaonline.org/articles/hindu, ilitazamiwa 6-05-2016
- ↑ Will Sweetman (2003), Mapping Hinduism: 'Hinduism' and the Study of Indian Religions, 1600-1776, Otto Harrassowitz Verlag, ISBN 3-931479498, pages 163, 154-168
Viungo vya Nje
hariri- Rigveda. Britannica Concise Encyclopedia Archived 7 Agosti 2004 at the Wayback Machine.
- "Hinduism" on Microsoft Encarta Online Archived 28 Februari 2005 at the Wayback Machine.
- Wiki based encyclopedia about Hindusim
- http://www.hinduism-today.com Archived 8 Januari 2009 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |