James Kirkwood (22 Agosti 192421 Aprili 1989) alikuwa mchezaji na mwandishi wa michezo ya kuigiza kutoka nchi ya Marekani. Anajulikana hasa kwa kuandika, pamoja na Nicholas Dante, igizo lenye muziki liitwalo kwa Kiingereza A Chorus Line lililotolewa 1975. Mwaka wa 1976 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Pulitzer ya Tamthiliya kwa ajili ya igizo hilo.

James Kirkwood
Amezaliwa James Kirkwood, Jr.
22 Agosti 1924
Los Angeles, Marekani
Amekufa 21 Aprili 1989
New York, Marekani
Nchi Marekani
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu James Kirkwood kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.