Jamhuri Jazz Band
Jamhuri Jazz Band ilikuwa bendi ya muziki wa dansi kutoka Dar es Salaam, Tanzania. Bendi ilianzishwa katika miaka ya 1950 hivi.
Jamhuri Jazz Band | |
---|---|
Jamhuri Jazz Band katika miaka ya 1950-60
| |
Maelezo ya awali | |
Asili yake | Dar es Salaam, Tanzania |
Aina ya muziki | Muziki wa dansi |
Miaka ya kazi | Miaka ya 1950 - |
Historia na mtindo wa uimbaji
haririBendi hii ilianza kwenye miaka ya 50 ikiwa ikijulikana kama Yanga Nyamwezi Band, Kiukweli ilikuwa ni Young Nyamwezi Band, bendi iliyokuwa imetengenezwa kwa ajili ya Vijana toka Tabora waliokuja kukata mkonge katika mashamba ya mkonge yaliyokuweko Tanga miaka hiyo. Na baada ya Uhuru ikajulikana kama Jamhuri Jazz Band, kifupi JJB japo kifupi hicho baadaye kilidaiwa kuwa kilikuwa kifupi cha jina mwenye bendi Joseph Bagabuje.
Wakati wa uhai wa Jamhuri Jazz bendi Tanga kulikuwa kuna waka moto kwa vikundi maarufu katika Afrika ya Mashariki kuwa vyote katika mji huo. Atomic Jazz, Amboni Jazz, Lucky Star, Black Star. Kwa vyovyote Tanga ulikuwa mji wa starehe wakati huo, hasa kwa kufuatia kuwa kulikuweko na bendi nyingine ambazo hazikuwa maarufu labda kutokana na aina ya muziki zilizokuwa zinapiga. Kama vile ile bendi ya Magoa The Love Bugs ambayo ndiyo hatimaye ilikuja kuwa The Revolutions na sasa Kilimanjaro Band.