Janeth Pangamwene

Mchezaji wa Mpira wa miguu Tanzania

Janeth Christopher Pangamwene (alizaliwa 27 Novemba 2000), ni mchezaji wa mpira wa miguu nchini Tanzania ambaye anacheza kama kiungo katika klabu ya Mlandizi Queens na timu ya Taifa ya wanawake Tanzania.

Janeth Christopher Pangamwene
Maelezo binafsi
Tarehe ya kuzaliwa 27 Novemba 2000
Mahala pa kuzaliwa    Tanzania
Nafasi anayochezea Kiungo
Timu ya taifa
Timu ya Taifa ya wanawake Tanzania

* Magoli alioshinda

Ushiriki Kimataifa hariri

Mnamo mwaka 2019, Pangamwene aliitwa kwenye Timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania chini ya miaka 20 kwa ajili ya ufunguzi wa michuano ya Kombe la COSAFA la Wanawake chini ya miaka 20 mwaka 2019.[1]Mwishoni mwa shindano hilo waliibuka mabingwa baada ya kuishinda Zambia kwa mabao 2-1 kwenye fainali.[2] Baadaye alipandishwa ngazi hadi upande wa timu ya wakubwa na aliteuliwa kwenye kikosi cha mashindano ya Wanawake ya Kombe la COSAFA 2020. Mwaka uliofuata, alitajwa katika orodha ya kikosi cha 2021 cha Mashindano ya Wanawake ya Kombe la COSAFA[3] Alicheza mechi nne wakati wa mashindano hayo huku Tanzania ikiibuka mabingwa kwa mara ya kwanza katika historia.[4]


Marejeo hariri

  1. "Twiga Stars news: Aisha Masaka and Irene Kisisa named in Cosafa U20 Women's Championship squad | Goal.com". www.goal.com. Iliwekwa mnamo 2022-03-02. 
  2. "Botswana, Zambia draw, meet in semis – Zambia Daily Mail". www.daily-mail.co.zm. Iliwekwa mnamo 2022-03-02. 
  3. "Tanzania go for youth at 2021 COSAFA Women's Championship". COSAFA. 20 September 2021.  Check date values in: |date= (help)
  4. Football, CAF-Confedération Africaine du. "Tanzania stop Malawi to win COSAFA Women's Championship 2021 title". CAFOnline.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-03-02. 
  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Janeth Pangamwene kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.