Jeanne Clare Adams
Jeanne Clare Adams (15 Juni 1921 – 21 Aprili 2007) alikua mwanasayansi wa kompyuta wa Marekani. Alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Viwango ya ANSI X3J3 Fortran[1] ambayo "ilitengeneza pendekezo lenye utata la Fortran 8X".Alihitimu Shahada ya Uzamili ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Michigan mnamo mwaka 1943, na MS katika mawasiliano ya simu na uhandisi wa umeme katika Chuo Kikuu cha Colorado mnamo mwaka 1979.
Nafasi yake ndefu zaidi aliyoshikilia ilikuwa katika Kituo cha Kitaifa cha Utafiti wa Anga, Boulder, Colorado, kuanzia mnamo mwaka 1960. hadi 1981, alihudumu kuanzia mnamo mwaka 1984 hadi 1997 kama naibu mkuu wa Kitengo cha Kompyuta. Adams pia alikuwa mwenyekiti wa Kamati ya Shirika la Viwango vya Kimataifa kuhusu Lugha za Kupanga (TC97/SC5), sasa ISO/IEC JTC 1/SC 7 na Kamati ya Viwango ya ANSI Fortran (X3J3).[2][3]
Marejeo
hariri- ↑ http://www.sternwarte.uni-erlangen.de/~ai05/vorlesungen/astrocomp/f77-standard.pdf
- ↑ Lee, J.A.N. "Computer Pioneers". IEEE Computer Society. Iliwekwa mnamo 20 Oktoba 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ John A. N. Lee; J. A. N. Lee (1995). International Biographical Dictionary of Computer Pioneers. Taylor & Francis. ku. 8–. ISBN 978-1-884964-47-3.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jeanne Clare Adams kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |