Jeff Koinange (alizaliwa 7 Januari 1966) ni mwandishi wa habari wa televisheni, anayejulikana kuwahi kufanya kazi CNN kama mwandishi wa habari za kutoka Afrika, na kwa CNN International mnamo 2001-2007.

Maisha hariri

Koinange alizaliwa nchini Kenya na alifanya kazi na kituo cha kwanza huru nchini Kenya: KTN (Kenya Television Network). Yeye alihudhuria Shule ya Kingsborough Community mjini Brooklyn, NY, kati ya 1987-1989 na kufuzu kwa kupata shahada. Yeye pia alipata shahada ya Sanaa katika utangazaji na uandishi wa habari kutoka Chuo Kikuu cha New York.

Kabla ya kujiunga na CNN, Koinange alifanya kazi kwa Reuters Television mnamo 1995-2001, akiripotia habari za Afrika na kufanya kama mtayarishaji mkuu mnamo 1999-2001. Yeye pia alifanya kazi kama mtayarishaji wa NBC News mwaka 1994 na pia aliwahi kufanya kazi kwa ABC News mmamo 1991-1992. Baada ya miezi saba ya kuacha kazi CNN, Jeff aliajiriwa kama mtangazaji habari wa kituo cha televisheni ya Kenya, K24, ambayo ilianza kufanya majaribio mjini Nairobi mnamo Desemba 2007. Yeye ni mtangazaji wa Capital Talk Show, inayofanana na Larry King Live (CNN).

Alipokuwa akifanya kazi CNN hariri

Miongoni mwa habari muhimu zaidi Koinange amewahi kuripotia barani Afrika alipokuwa CNN ni mgogoro ya Darfur vita vya wenyewe kwa wenyewe mchini Liberia na Sierra Leone na njaa nchini Niger, ambayo Koinange alishinda tuzo la Emmy.

Mapema mwaka 2007, Koinange alikanywa na serikali ya Nigeria kuhusu ripoti yake ya [1] Movement for the Emanicipation of the Niger Delta (MEND). Katika ripoti yake, Koinange aliwafuata MEND waliojifunika uso mpaka kwa kambi ambapo walikuwa wamewateka nyara watu wa Ufilipino. Serikali ya Nigeria ilisema kuwa ripoti hiyo ilikuwa "ya uwongo", na CNN inakanusha madai hayo.

Koinange pia ameripotia habari nje ya Afrika, kama ripoti yake ya wimbi la Hurricane Katrina na vilevile vita vya Iraq. [2]

Mnamo 29 Mei 2007, CNN ilitangaza kuwa Koinange hafanyi tena kazi na wao. Inadaiwa kuwa alikuwa amepatikana na kashfa ya ngono ambayo CNN haikutaka kujihusisha nayo.[3]

Marejeo hariri

  1. Koinange, Jeff (10 Februari 2002). [1]Koinange: Big bunduki, big yanapogongana mafuta nchini Nigeria. CNN
  2. Staff taarifa (Spring 2006). [2] Archived 14 Juni 2007 at the Wayback Machine. Albamu imetoa Kingsborough Intrepid Habari CNN, Jeff Koinange Archived 14 Juni 2007 at the Wayback Machine. CUNY Matters.
  3. Jeff Koinange No Longer Employed By CNN. Archived 1 Juni 2007 at the Wayback Machine. TVNewser via mediabistro

Viungo vya nje hariri