Reuters

shirika la habari la kimataifa

Reuters ni shirika la habari linalomilikiwa na Thomas Reuters[1] Ni kati ya vyombo vya habari vikubwa na vinavyoaminiwa sana ulimwenguni.[2]

Alternative text
Reuters London
Nembo ya Reuters (imetolewa 2020)

Shirika hili limeajiri waandishi wa habari takriban 2500 na wapiga picha habari wapatao 600 waliosambazwa kwenye vituo 200 katika maeneo mbalimbali ya dunia na kuripoti katika lugha 16 tofauti.[3]

Shirika hili liliasisiwa jijini London mnamo mwaka 1851 na mtu mwenye asili ya Ujerumani, Paul Reuters. Baadaye lilinunuliwa na Thomson Corporation ya Canada mnamo mwaka 2008 na sasa limekuwa tawi linaloshughulika na habari la kampuni kuu ya Thomson Reuters.[4]

Historia

hariri

Karne ya 19

hariri
 
Paul Reuter, mwasisi wa Reuters (picha iliyopigwa na Nadar, mwaka 1865)

.

Paul Reuter alikuwa akifanya kazi kwenye kampuni ya uchapishaji wa vitabu ya mjini Berlin na alijihusisha na usambazaji wa majarida ya watu wenye misimamo mikali nyakati za mwanzoni mwa Mapinduzi ya 1848. Machapisho hayo yalimfanya Reuters kufikiri sana, na mnamo mwaka 1850 akaanzisha shirika lake la habari kama majaribio huko Aachen akitumia utaratibu wa usambazaji wa nyumba kwa nyumba na telegramu kuanzia 1851 na kuendelea, ili kutuma arafa baina ya Brussels na Aachen,[5] kwenye mtaa ambao leo una Jumba la Reuters la Aachen.

Tanbihi

hariri
  1. "Thomson Reuters | History & Facts | Britannica.com". web.archive.org. 2018-11-07. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-11-07. Iliwekwa mnamo 2024-10-09.{{cite web}}: CS1 maint: bot: original URL status unknown (link)
  2. Reuters
  3. Reuters
  4. Stephen Brook (30 Mei 2006). "Reuters recruits 100 journalists". The Guardian. Iliwekwa mnamo 5 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Wynter, Andrew (1861). Our social bees; or, Pictures of town & country life, and other papers. United Kingdom: R. Hardwicke. uk. 298. Iliwekwa mnamo 14 Agosti 2023.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)