Jennifer Abel
Jennifer Abel. (amezaliwa 23 Agosti 1991)) ni mpiga mbizi wa Kanada. Kwa sasa anashirikiana na Mélissa Citrini-Beaulieu kwa upigaji mbizi. Alishinda medali ya shaba ya Olimpiki kwenye Olimpiki ya Mwaka 2012 katika mbio za mita 3, tukio la kupiga mbizi la synchro na Émilie Heymans na medali ya fedha katika Olimpiki ya Mwaka 2020 akiwa na Melissa Citrini-Beaulieu. Abel ni bingwa mara nne wa Michezo ya Jumuiya ya Madola katika mashindano ya mita 1 na 3, na pia ni bingwa mara tatu wa Michezo ya Pan American katika mashindano ya mita 3 na mita 3. Katika Medali zake kumi (sita za fedha, nne za shaba) katika Mashindano ya Dunia ya FINA ni rekodi aliopata medali nyingi zaidi na ni Mkanada wa kwanza, kupata Medali hizo katika kupiga mbizi kwenye mashindano ya dunia.
Abel alikua mmoja wa wapiga mbizi wachanga zaidi nchini Kanada alipofanya Olimpiki yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 16 katika Olimpiki ya Majira ya joto mwaka 2008.[1] Ingawa alishindwa kushinda medali katika michezo ya Olimpiki mwaka huo, Abel alipata mafanikio pamoja na mwenzake Emilie Heymans kwenye mzunguko wa Grand Prix, na kushinda medali kadhaa.[2] Kazi yao kwa pamoja ingeendelea baada ya hapo, na Abel angefaidika zaidi kutokana na uzoefu wa Heymans ambapo angepata medali nyingi za Grand Prix hadi 2010.
Marejeo
hariri- ↑ "Diving Plongeon Canada -Jennifer Abel". web.archive.org. 2011-10-01. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-10-01. Iliwekwa mnamo 2021-12-03.
- ↑ "Jennifer Abel". Team Canada - Official Olympic Team Website (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-12-03.