Jeshi la ardhi
Jeshi la ardhi ni mkono wa jeshi la nchi unaojumlisha vikosi vyote vilivyo tayari kupigania maadui kwenye nchi kavu, tofauti na mikono mingine inayoshughulika kazi ya ulinzi wa taifa baharini (jeshi la majini) au hewani (jeshi la anga).
Watu kwenye jeshi la ardhi huitwa askari au wanajeshi. Hupangwa kwa vikosi mbalimbali wakitumia silaha na vifaa kama vile bunduki, mizinga, vifaru, helikopta na mengine.
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |