Jimeta ni mji mkubwa katika jimbo la Adamawa nchini Nigeria. Mji umekadiriwa kuwa na wakazi lakhi mbili na nusu mwaka 2005. Uko kando ya mto Benue ukitazama [Kameruni].

Shule ya Shima Elementary iliyopo ndani ya mji wa Jimeta
Shule ya Shima Elementary iliyopo ndani ya mji wa Jimeta

Kwa miaka kadhaa wakati wa ukoloni uliunganishwa na mji wa karibu wa Yola lakini tangu mwaka 1955 umekuwa tena mji wa pekee.

Jimeta ni bandari muhimu kwenye njia ya mto Benue. Hasa wakati wa maji mengi kati ya Julai hadi Oktoba meli ndogo hubeba karanga na pamba kutoka Kameruni pamoja na ngozi kutoka Adamawa kwenda mabandari ya baharini kwenye mdomo wa mto Niger.

Jimeta imeunganishwa kwa barabara na Yola, Bombi, Mubi, Bama, and Maiduguri. Kuna feri kwenda Kamerun.