Bandari ni mahali pa kupokea meli na kuhamisha mizigo yao pamoja na abiria. Bandari inatakiwa kuipa meli kinga dhidi ya mawimbi makubwa na vifaa ya kupakiza au kutoa mizigo. Kuna mabandari asilia na mabandari yaliyotengenezwa kwa kusudi hii. Kwa jumla bandari ni sehemu muhimu za miundombinu wa nchi.

Mabandari makubwa ya dunia
Kwenye bandari ya Singapur
Bandari ya Hamburg huwa na winchi za upakizaji za kisasa kabisa

Mabandari hutengenezwa kando la bahari, maziwa au mito.

Kati ya sifa muhimu kwa ajili ya bandari ni

 • kina cha maji cha kutosha kulingana na ukubwa wa meli zinazoitumia.
 • mitambo kama winchi za upakizi
 • nafasi za ghala
 • njia za usafiri kama reli na barabara za kusafirisha mizigo

Mabandari hutofautiana kulingana na kusudi lao na aina za mizigo inayoshughulikiwa humo.

Mabandari madogo zinahudumia wavuvi au jahazi za burudani.

Kuna mabandari yanayopokea mizigo ya kila aina kama bandari ya Dar es Salaam au Mombasa.

Mara nyingi kuna mabandari yanayoshughulika mizigo maalumu kama mafuta, kontena, kivuko na kadhalika.

Mabandari yanayoshughulika mizigo mingi duniani

(mizigo kwa mwaka tani milioni)

 1. Shanghai (Jamhuri ya Watu wa China) 537,0
 2. Singapur 448,2
 3. Rotterdam (Uholanzi) 378,2
 4. Ningbo (Jamhuri ya Watu wa China) 300,0
 5. Guangzhou (Jamhuri ya Watu wa China) 300,0
 6. Tianjin (Jamhuri ya Watu wa China) 255,0
 7. Hong Kong (Jamhuri ya Watu wa China) 238,0
 8. Nagoya (Japani) 206,0
 9. Qingdao (Jamhuri ya Watu wa China) 200,0
 10. Dalian (Jamhuri ya Watu wa China) 200,0
 11. Antwerpen (Ubelgiji) 167,4
 12. Los Angeles (USA) 162,1 (2005)
 13. Durban (RSA) 104,8
 14. Mombasa (EACU) 100,2
 15. Port Suez (Misri) 80,2
 16. Abidjan (Cote d'Ivoire) 50,6

Mabandari yanayoshughulika na mizigo, bandari huru na usafiri duniani

AS

 1. Singapur
 2. Chiba
 3. Inchon

AF

 1. Port Suez
 2. Kivukoni
 3. Dauola
 4. Beneficae

AM

 1. Halifax
 2. Toronto
 3. Oakland San Fransico
 4. Boston
 5. New York

EU

 1. Antwep
 2. Porto

LA

 1. Rio de Janairo
 2. Havana

ME

 1. Dubai
 2. Boophurus
 3. Nhava Shiva

{{mbegu-uchumi na usafiri}