Benue (mto)

(Elekezwa kutoka Mto Benue)

Mto Benue (kwa Kifaransa: Bénoué) ni tawimto kubwa la mto Niger. Chanzo chake ni katika nyanda za juu za Kamerun, hasa milima ya Adamawa.

Mto wa Benue
Mto wa Benue karibu na Jimeta kati ya Nigeria na Kameruni
Mto wa Benue karibu na Jimeta kati ya Nigeria na Kameruni
Chanzo Nyanda za juu za Adamawa katika Kamerun
Mdomo Niger
Nchi za beseni ya mto Kameruni na Nigeria
Urefu 1,400 km
Kimo cha chanzo 1,34 m kwa 7°40'N 13°15'E
Kiasi cha maji kinachotolewa mdomoni 2,400 m³/s
(wastani ya miaka ya 1980)
Eneo la beseni (km²) ?? km²

Katika sehemu ya kwanza ya mwendo wake unatelemka mita 600 kwa mwendo kali. Karibu na mji wa Garua unaungana na mto Mayo Kébi. Baada ya mwendo wa km 350 mto huo unatoka Kamerun na kuingia Nigeria karibu na bandari ya Jimeta. Huko mto una upana wa kilomita moja unaoweza kupanua wakati wa mvua. Baada ya Yola mto unapokea tawimto lake muhimu zaidi, mto Gongola.

Katika Nigeria mto ni njia muhimu ya kusafirisha mizigo na mazao ya nchi kati ya pwani ya Atlantiki na sehemu za bara.

Unaishia katika mto Niger kwenye mji wa Lokoja.

Tazama pia

hariri

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Benue (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.