Joênia Batista de Carvalho alizaliwa tarehe 20 April 1974 ni Wakili wa kwanza mwenye asili ya nchini Brazil na Mwanachama wa kabila la Wapixana kaskazini mwa Brazil. Baada ya kuleta mzozo wa ardhi mbele ya Tume ya Haki za Binadamu ya Kimataifa linalojulikana kama Inter-American Commission on Human Rights, Wapixana alikuwa wakili wa kwanza wa asili kutoa hoja mbele ya Mahakama Kuu ya Brazil. Yeye ni rais wa sasa wa Tume ya Kitaifa ya Ulinzi wa Haki za Watu wa Asili. Alichaguliwa kuwa mwakilishi wa shirikisho kwa jimbo la Roraima, kupitia orodha ya chama cha Mtandao wa Uendelevu (REDE), katika uchaguzi mkuu wa 2018. Batista de Carvalho ni mwanamke wa kwanza wa asili aliyechaguliwa katika Bunge la Wawakilishi na mbunge wa pili wa asili tangu uchaguzi wa Mário Juruna mwaka 1982.[1] Baada ya Luiz Inácio Lula da Silva kuingia madarakani kama Rais wa Brazil, yeye akawa Rais wa FUNAI na pia Mwanamke wa kwanza wa asili kushika jukumu hilo. [2]

Maisha ya Awali

hariri

Joênia alizaliwa katika jimbo la Roraima nchini Brazil na alikulia katika vijiji vilivyotengwa kama Truarú au Guariba katika eneo la Amazon, ambapo njia za maisha za jadi zilistawi na wazee wachache walizungumza lugha ya Kireno. Wakati wazazi wake walipelekwa kutoka kijiji chao kuandikisha kuzaliwa kwao na watoto wao, karani alichagua jina rasmi Joênia Batista de Carvalho kwa ajili ya nyaraka zake za kitambulisho. Yeye hujitambulisha kwa jina lake la kwanza na uhusiano wake wa kabila kama Joênia Wapixana. Kufikia umri wa miaka saba au nane, baba wa Joênia alikuwa ameondoka katika familia na Mama yake alihamia Mji mkuu wa jimbo, Boa Vista, akitafuta fursa za kiuchumi.Watoto walijiandikisha shuleni, ingawa ndugu zake watatu wakubwa waliacha shule ili kwenda kufanya kazi. Joênia alimaliza masomo yake ya sekondari katika miaka ya 1990 na awali alifikiria kuwa daktari, kwani hakuwa na nia ya njia kawaida ya wanawake wa asili walioelimika, kufundisha. Alijiandikisha katika chuo cha sheria, huku akifanya kazi usiku katika ofisi ya uhasibu kulipia masomo yake. Mwaka 1997, Joênia alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Shirikisho cha Roraima (UFRR) akiwa wakili wa kwanza wa asili nchini Brazil.

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Joênia Wapixana kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.