Kireno (Português - tamka "purtuGESH") ni lugha ya Kirumi inayozungumzwa hasa nchini Ureno na Brazil, lakini pia Kusini mwa Afrika, Asia Kusini na Asia Kusini-Mashariki.

Nchi penye Kireno kama lugha rasmi

Imekuwa lugha ya kimataifa kutokana na historia ya ukoloni ya Ureno ikiwa na wasemaji wa lugha ya kwanza milioni 210-215; pamoja na wasemaji wa lugha ya pili kuna watu milioni 270 duniani wanaoelewana kwa Kireno, hivyo ni lugha ya 5 au ya 6 ulimwenguni.

Kutokana na historia ya ukoloni Kireno kimepatikana katika nchi zifuatazo:

Kireno kama lugha rasmi hariri

Lugha ya kieneo hariri

Historia ya lugha hariri

Kireno ni moja kati ya lugha za Kirumi maana yake kimetokana na Kilatini cha Dola la Roma lililotawala eneo la Ureno kwa karne nyingi.

Ni karibu hasa na Kigalicia kinachozungumzwa katika Hispania ya Kaskazini.

Wareno waliacha lugha yao katika makoloni yao. Leo hii idadi ya wasemaji katika Ureno ni milioni 10 tu - idadi kubwa kabisa wako nje ya Ureno, hasa Brazil.

Kireno kilisambaa zaidi katika karne ya 20 kwa sababu Wareno waliondoka Ureno kutafuta kazi katika nchi nyingi za Ulaya. Vilevile kuna Wabrazil na Waangola waliotoka kwao kuhamia penginepo wakienda na lugha yao.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kireno kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.