Johannes Willebrands
Johannes Gerardus Maria Willebrands (Bovenkarspel, Kaskazini mwa Uholanzi, 4 Septemba 1909 – 1 Agosti 2006) alikuwa Kardinali wa Kanisa Katoliki kutoka Uholanzi. Alikuwa Rais wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Kikristo kutoka mwaka 1969 hadi 1989, na Askofu Mkuu wa Utrecht kutoka mwaka 1975 hadi 1983. Aliteuliwa kuwa Kardinali mwaka 1969.
Willebrands alikuwa na mchango mkubwa katika kukuza ekumeni (umoja wa madhehebu) katika Kanisa katika nusu ya pili ya karne ya 20, na alionekana kama mmoja wa wagombea wa kiti cha upapa katika makongamano mawili ya uchaguzi wa papa yaliyofanyika mwaka 1978. [1]
Marejeo
hariri- ↑ Salvador Miranda. "Cardinals camerlengo of the Sacred College of Cardinals". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 25 Mei 2009.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |