Ekumeni ni tapo la Ukristo linalolenga kurudisha umoja kamili kati ya madhehebu yake mbalimbali.

Alama ya ekumeni ni boti lenye msalaba kati ya bahari.[1]

Msingi wake ni imani inayowaunganisha katika Yesu Kristo na kwa njia yake katika Utatu mtakatifu, yaani Mungu pekee aliye Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

Neno linatokana na Kigiriki oikouméne, linalomaanisha kwa asili sehemu ya dunia iliyokaliwa na watu; hivyo likaja kuwa na maana ya jambo linalohusu waamini duniani kote.

Ekumeni ilianza kati ya Waprotestanti, hasa lilipofanyika Kongamano la Kimisionari la Kimataifa huko Edimburg, mwaka 1910, ambapo waliohudhuria walisisitiza uhusiano kati ya umoja wa Wakristo na kazi ya uinjilishaji wa mataifa yote.

Mwaka 1937 iliundwa Halmashauri ya Kiekumeni ya Makanisa, ikijumlisha hata Waorthodoksi. Kwa sasa inawakilisha robo tu ya Wakristo wote, kwa sababu Wakatoliki na Wapentekoste wengi hawajajiunga na muundo huo.

Hata hivyo Kanisa Katoliki liliingia kwa nguvu katika juhudi za ekumeni kuanzia Papa Yohane XXIII (1958-1963) na Mtaguso wa pili wa Vatikano (1962-1965).

Tanbihi hariri

  1. Logo. World Council of Chuches. Iliwekwa mnamo 6 August 2016.
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ekumeni kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.