John Njoroge Michuki
John Njoroge Michuki (* 1932) ni mfanyabiashara na mwanasiasa nchini Kenya.
Michuki ni mwenyeji wa wilaya ya Muranga alikozaliwa katika familia ya Wakikuyu. Alisoma A-levels huko Mangu High School pamoja na Mwai Kibaki halafu uchumi kwenye chuo kikuu cha Oxford (Uingereza).
Kati ya 1970 na 1979 alikuwa mwenyekiti wa Kenya Commercial Bank.
1983 alijiunga na siasa akiwa mbunge wa KANU kwa Kangema [1] na kupewa vyeo mbalimbali serikalini.
Kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1992 akajiunga na chama cha upinzani Ford-Asili akarudishwa bungeni tena mwaka 1997 kwenye tiketi ya Ford-People.
2002 alisimama upande wa NARC akaingia katika serikali ya kwanza ya rais Mwai Kibaki kama waziri wa usafiri na uchukuzi. Alikuwa maarufu kwa ukali jinsi alivyowalazimisha wenye matatu na madereva kutii utaratibu wa barabarani pamoja na kuweka mitambo ya kupakana mkasi wa mwendo wa gari na kanda za usalama.
2005 akawa waziri wa usalama wa ndani. Katika kipindi hiki alipata sifa mbaya kwa kuamuru uvamizi wa ofisi za gazeti la East African Standard pamoja na kituo cha televisheni cha KTN. Vilevile mauaji ya watu wengi walioangaliwa kuwa wafuasi wa kundi la Mungiki yalihesabiwa kuwa yalitokea chini ya mamlaka yake Michuki.
Katika serikali ya Januari 2008 Michuki amekuwa waziri wa barabara na kazi za umma.
Viungo vya Nje
hariri- ↑ Center for Multiparty Democracy: Politics and Parliamentarians in Kenya 1944-2007 Archived 28 Februari 2008 at the Wayback Machine.
- The Standard, 8 Desemba 2005: Kibaki’s new cabinet Archived 23 Februari 2008 at the Wayback Machine.
- http://www.statehousekenya.go.ke/government/cvs/johnmichuki.htm Archived 27 Aprili 2006 at the Wayback Machine.
- http://www.parliament.go.ke/MPs/members_michuki_n.php Archived 27 Septemba 2007 at the Wayback Machine.