José Luis Escobar Alas
José Luis Escobar Alas (alizaliwa Suchitoto, wilaya ya Cuzcatlán, 10 Machi 1959) ni Askofu Mkatoliki wa Salvador ambaye amehudumu kama Askofu Mkuu wa San Salvador tangu 2009.
Escobar aliwahi kuwa Askofu wa San Vicente kuanzia mwaka wa 2005, kabla ya kupandishwa cheo huko San Salvador tarehe 27 Desemba 2008. Hapo awali alikuwa askofu msaidizi katika Jimbo la San Vicente tangu 2002, baada ya kuingia ukuhani mwaka 1982.
Wasifu
haririEscobar alisomea upadre katika Seminari ya San José de la Montaña huko San Salvador kabla ya kuingia Seminari ya Meya de Morelia huko Mexiko. Baadaye alihitimu shahada ya falsafa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian, Roma. Tarehe 15 Agosti 1982 alipewa daraja la Upadre.[1][2]
Marejeo
hariri- ↑ Salvadoran Bishops' Conference info (Spanish) Archived 2008-11-20 at the Wayback Machine
- ↑ "Salvadoran Archbishop Praises Government Crackdown on Gangs". Associated Press (kwa Kiingereza). 31 Julai 2022. Iliwekwa mnamo 23 Agosti 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |