Askofu msaidizi (kwa Kiingereza "auxiliary bishop") ni kiongozi wa Kikristo aliyeteuliwa hasa kwa lengo la kwamba amsaidie askofu wa jimbo kuongoza na kusimamia jimbo lake kulingana na mwongozo wake.

Maaskofu waliokusanyika katika Mtaguso wa kwanza wa Nisea

Katika Kanisa Katoliki

hariri

Ili kufikia lengo hilo kwa kawaida anateuliwa kuwa makamu wa askofu (walau mmojawao ikiwa maaskofu wasaidizi ni zaidi ya mmoja).

Upande wa sakramenti askofu msaidizi ni askofu kamili aliyepewa daraja takatifu ya juu kama walivyo maaskofu wengine na huweza kutoa sakramenti zote zikiwa ni pamoja na daraja takatifu ila atahitaji ruhusa ya askofu wa jimbo ili kufanya hivyo (au ya Papa ili kutoa ile ya uaskofu).

Kwa kuwa yumo katika urika wa maaskofu, ni haki yake kushiriki mtaguso wowote utakaofanyika katika eneo lake na hata mtaguso mkuu.

Katika Kanisa Katoliki la Magharibi askofu msaidizi huteuliwa na Papa kwa ombi la askofu wa jimbo, ambaye ana pendekeza majina matatu ya mapadri.

Kati ya majimbo yenye maaskofu wasaidizi wengi zaidi, kuna yale ya Mexico City, Roma, Milano, Chicago, Buenos Aires, Rio de Janeiro, Sao Paulo na Los Angeles.

Viungo vya nje

hariri